Viongozi wapya KAAT na viongozi wa zamani wakipongezana mara baada ya uchaguzi huo.
Makamu wa Rais wa KAAT aliyemaliza muda wake, Bibi Margaret Alfanies (Katikati) akizungumza machache mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi huo. Kushoto ni aliyekuwa Muweka Hazina wa KAAT, Bibi Emilia Maingu na kulia ni Bw. Stephen Matee ambaye ni Muweka Hazina mpya.
Makamu wa Rais wa KAAT aliyemaliza muda wake, Bibi Margaret Alfanies (Wapili Kulia) akikabidhi nyaraka za KAAT kwa uongozi mpya. Kutoka kushoto pichani ni Bw. Emmanuel Burton (Makamu wa Rais, Tanzania Bara), Bw. Bukheti Juma (Wapili kushoto) ambaye ni Makamu wa Rais, KAAT (Zanzibar). Wengine ni Rais Mpya Bw. Stephen Katemba (Katikati) na Bw. Stephen Matee (Kulia)ambaye ni Muweka Hazina mpya.
Uongozi mpya wa KAAT wakizungumza na Mwakilishi Mkazi wa KOICA, Bw. Seung-Beom Kim (Wapili kulia).
Wakiwa katika picha ya pamoja ni uongozi mpya wa KAAT na baadhi ya viongozi wa zamani wa Jumuiya hiyo.
------------------------------------------
Na Saidi Mkabakuli
Jumuiya ya Watanzania waliosoma
Korea imefanikiwa kupata uongozi mpya, utaongoza umoja wa Watanzania hao kwa
muda wa miaka miwili.
Waliochaguliwa kuongoza KAAT ni
pamoja na Bw. Stephen Katemba ambaye amechaguliwa kuwa Rais wa Jumuiya. Bw. Katemba
atasaidiwa na Bw. Bukheti Juma (Makamu wa Rais, Zanzibar) na Bw. Emmanuel
Burton (Makamu wa Rais, Tanzania Bara). Katika nafasi ya Uweka Muweka Hazina,
aliyechaguliwa ni Bw. Stephen Matee, ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa
Fursa Sawa kwa Wote (EOTF) ulio chini wa Mama Anna Mkapa.
Akizungumza mara baada ya
kukabidhiwa rasmi jukumu la kuiongoza Jumuiya hiyo, Bw. Katemba ambaye ni
Mtaalamu wa Masuala ya Uchumi na Biashara za Kimataifa, amesema kuwa Tanzania
ina fursa kubwa katika eneo la biashara za kimataifa kuwa kuzingatia rasilimali
zilizopo nchini na kuchagiza kuwa fursa hizo zinaweza kutumiwa ipasavyo kwa
kujitangaza tu.
Bw. Katemba aliongeza kuwa kama
Watanzania tukiwa na uzalendo wa dhati na kuwa mabalozi wazuri, Tanzania
itakuwa na uhakika wa kukamata masoko makubwa ikiwemo Korea na Bara la Asia kwa
ujumla.
“Kwa mfano kwa mujibu wa hali
ya uchumi wa Taifa, kwa mwaka 2013, mwenendo wa biashara ya bidhaa na huduma
nje haukuwa wa kuridhisha ikilinganishwa
na ilivyokuwa mwaka 2012. Thamani ya mauzo ya bidhaa na huduma nje ilipungua
kwa asilimia 1.7 kutoka Dola za Kimarekani milioni 8,675.6 mwaka 2012 hadi Dola
milioni 8,532.0,” alisema.
Kwa mujibu wa Bw. Katemba kuwa
ili kufikia malengo ya kimkakati ya Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano ulio
chini ya Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ambao umelenga kufungulia fursa za
ukuaji wa uchumi, Tanzania haina budi kufikia malengo ya kikao cha tisa cha Shirikisho
la Biashara Ulimwenguni (WTO) ambalo linalenga kuziwezesha kibiashara nchi
wanachama kuboresha biashara zao.
“Katika kikao cha tisa cha WTO,
Mawaziri wa nchi wanachama 159 wa Shirikisho walikubaliana kuwa na “Mpango wa Bali” ambao
unalenga kuziruhusu nchi zinazoendelea kuwa na fursa zaidi ya kuzalisha chakula
cha akiba, kuinua kiwango cha biashara kwa nchi changa na kusaidia maendeleo ya
nchi changa kibiashara. Hivyo, tunaweza kufikia malengo haya kwa kutangaza
bidhaa zetu hasa za vyakula kwa mataifa yenye uhitaji wa bidhaa hizo,”
alifafanua.
Akizungumza wakati wa mkutano
huo, Mwakilishi Mkazi wa KOICA, Bw. Seung-Beom Kim alisema kuwa Tanzania ina
bidhaa nyingi ya kuziuza kwenye soko la Korea na kutolea mfano mchele wa Kyela
kuwa ni bidhaa nzuri kwenye soko hilo.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269