Breaking News

Your Ad Spot

Jul 20, 2014

KISHOKA WA TANESCO LADAKWA LIVE MLIMANI, DAR ES SALAAM

10500539_819006161445574_7780628803053090260_n
Na Mwandishi wetum Dar esSalaam
Jamaa linalodaiwa kuwa tapeli lililokubuhu kwa masuala ya kulaghai watu kwa njia ya kujifanya kishoka wa Shirika la Umeme Nchini, Tanesco, jana asubuhi limedakwa baada ya kuwekewa mtego alipokuwa wakitaka kutapeli kwa mmoja wa Afisa wa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Usia Nkhoma- Ledama.

Akieleza tukio hilo Bi. Usia,, alidai kuwa tapeli huyo alifika asubuhi akiwa na wenzake sita, nyumbani kwake wakasema wanatoka Tanesco wamekuja kucheki mita ya Luku. Hata hivyo wakakorokocha wakasema mita imechezewa kwa hiyo wanakata Umeme na kung'oa mita, eti waliona kwenye GPS yao kuwaUmeme hauendi vema.

“wakasema fidia na kurudisha umeme kiofisi ni milioni 8! ila tukiwapa milioni 2 wataturudishia. nikawauliza kama mita imechezewa mbona tunanunua umemewa laki 3 kwamwezi? si ingepaswa tulipe kidogo? wakasema wakati mwingine wakiweka hiyo resistance (eti ndo kifaa cha kuiba Umeme) huwa kinafyatuka halafu Umeme unakwenda zaidi! “ alielezea Bi. Usia.

Na kuongeza kuwa vishoka hao wakakata Umeme wakaondoka, tujipange. tujadiliana na mzee tukapata mashaka maana walikuwa wakali halafu wanalazimisha mambo, wamevaa vitambulisho lakini wamevigeuza kwahiyo havisomeki. tukapiga simu Tanesco kuwauliza wakasema hao ni vishoka tuitePolisi, basi tukawapigia simu waje wachukue laki tano waturudishie Umeme, mengine Jumatatu. wakaja fasta wakarudisha Umeme, nikawaambia naenda aTM wasubiri nikawaacha na mzee nikatoka mbio mpaka Polisi chuo nikawahadithia wakanipa Polisi 3 nikaja nao nyumbani, tukawakuta wameondoka.

Mzee akawapigia simu waje hela imepatikana wakasema tukutane Mlimani City, tukafanikiwa kukamata mmoja wengine wakakimbia. tumemuacha selo, tukaandikisha maelezo. tunasubiri hatua itakayofuata.
10417599_819006198112237_2101442257557265538_n  
Hapa likiwa chini ya ulinzi na pingu mkononi.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages