WAJERUMANI WALIKABA MPAKA KIVULI CHA LIONEL MESSI, KWA `STAILI` HII KUISOMA NAMBA ILIKUWA LAZIMA TU`!
Nyota wa mvuto: Mechi ya fainali ya
kombe la dunia katika dimba la Maracana ilikuwa mechi kubwa zaidi katika
maisha ya soka ya Lionel Messi.
MCHEZAJI bora wa dunia mara nne
mfululizo, Lionel Messi aliibeba Argentina mabegani mwake katika mchezo
wa fainali dhidi ya Ujerumani usiku wa leo na kushuhudia nchi yake
ikipigwa bao 1-0 na kukosa ubingwa.
Mamilioni ya Waargentina walifurika Rio
de Janeiro wakiwa na matumaini makubwa ya kumuona shujaa wao Messi
akikata kiu yao ya kutaka ubingwa, lakini mambo yamekwenda ndivyo
sivyo.
Mabeki wa Ujerumani walicheza ngado kwa ngado na Messi na hawakutaka kumuachia hata upenyo.
Mtu wa kukabwa: Messi alikuwa chini ya
ulinzi wa wachezaji watatu wa Ujerumani na mpira ulichukuliwa na kiungo
fundi Bastian Schweinsteiger.
Mtu pekee: Picha iliyomuonesha Messi
akiwa amezingirwa na wachezaji watatu wa Ujerumani, ilikumbusha enzi za
gwiji wa pekee nchini Argentina, Diego Maradona ambaye alikuwa chini ya
msitu wa wachezaji wa Ubelgiji katika fainali za mwaka 1982.
Messi akichuana kupata mpira baada ya kufanikiwa kuipenya ngome ya ulinzi ya Ujerumani.
Analindwa: Messi akiwa amezingirwa na wachezaji wanne wa Ujerumani , huku akijaribu kutengeneza shambulizi la Argentina.
Haijatimia: Ameshindwa kuandika historia baada ya kushuhudia nchi yake ya Argentina ikipigwa kidude kimoja na Ujerumani.
UJERUMANI BINGWA KOMBE LA DUNIA
Mabingwa 2014: Nahodha wa Ujerumani, Philipp Lahm (wa pili kulia mbele) akinyanyua kombe la dunia na kushangilia .
Wachezaji wa Ujerumani wakishangilia baada ya kutwaa kombe la dunia katika dimba la Maracana kwa kuifunga Argentina bao 1-0.
Big Bosi: Kocha wa Ujerumani, Joachim Low (katikati) akinyanyua Kombe la Dunia
LIONEL MESSI AIBUKA KIDUME TUZO YA MCHEZAJI BORA KOMBE LA DUNIA 2014
Lionel Messi amepewa tuzo ya mchezaji bora wa mashindano .
LICHA ya kupoteza mechi ya fainali na
kukosa kombe la dunia mwaka 2014, mshambuliaji wa Argentina na
Barcelona, Lionel Messi ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa michuano ya
kombe la dunia mwaka huu nchini Brazil.
Tuzo hii imekuja kaka ya kustaajabisha kwa watu wengi, lakini kwa kiasi kikubwa alistahili kupewa.
Messi alionesha kiwango kikubwa katika
hatua ya makundi akifunga mabao 4 katika michezo mitatu dhidi ya
Bosnia, Iran na Nigeria, lakini nyota yake ilififia baada ya kushindwa
kufunga katika mechi za mtoano dhidi ya Switzerland, Ubelgiji, Uholanzi
na Ujerumani.
Katika mchezo wa fainali dhidi ya
Ujerumani, Messi alipoteza nafasi moja muhimu, lakini muda mwingi
alifanya jitihada za kutafuta upenyo bila mafanikio.
Lionel Messi alipiga shuti, lakini alikosa bao katika mchezo wa fainali Maracana.
Baada ya kipyenga cha mwisho, Messi alipokea tuzo yake ya mchezaji bora akiwashinda nyota wa Colombia James
Rodriguez, winga wa Uholanzi, Arjen Robben na wachezaji watatu wa
Ujerumani, Manuel Neuer, Bastian Schweinsteiger na Thomas Muller.
Ndoto zimezima: Lionel Messi akiangalia chini baada ya kupoteza mechi ya fainali dhidi ya Ujerumani.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269