Breaking News

Your Ad Spot

Jul 11, 2014

PINDA AKUTANA NA WATANZANIA WAISHIO READING UINGEREZA

 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe Tunu  (kulia) wakiongozana na Madona Pemba (kushoto) , mtanzania aishie Uingereza kuelekea kwenye ukmbi wa mikutano  ili kuzungumza na watanzania waishio Reading Julai 10, 2014.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe Tunu  (kulia) wakisalimiana na baadhi ya watoto na wazazi  waliohudhuria mkutano kati yake na watanzania waishio Reading Uingereza Julai 10, 2014.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akipokea zawadi ya mipira  kutoka kwa watanzania waishio Reading nchini Uingereza  kabla ya kuzungumza nao Julai  10, 2014. Kushoto ni Mwenyekiti wa Umoja wa Watanzania waishio Reading, Hussein Chang'a.
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe Tunu wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watanzania waishio Uingereza walioshiriki katika mkutano wake uliofanyika Reading Julai 10, 2014.
 Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda  (kushoto) akizungumza na mchungaji Kallaghe wa Kanisa la  Kiinjili la Kilutheri, maalum kwa Ibada za Kiswahili nchini Uingereza baada ya mkutano kati ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na watanzania waishio Reading  Julai 10 2014
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda Kizungumza na baadhi ya watanzania washio Reading Uingereza baada kufanya  nao mkutano  Julai 10, 2014. Kutoka kushoto ni Maina Owino, Madona Pemba na Diana Mathew. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages