MOROGORO, Tanzania
MAMLAKA ya Maji safi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) inatarajiwa kulipa karibu sh. Bilioni 8 kwa wananchi wanaoisho karibu na bwawa la Kidunda, Morogoro.
Mkurugenzi wa fedha wa DAWASA Didas Mwilawi alisema hayo leo wakati
wa kikao cha watendaji wa Mamlaka hiyo na Halmashauri ya wilaya ya Morogoro.
Amesema
fedha hizo zitalipwa kwa utaratibu wa hundi
kwa wananchi wote ambao tayari
walishahakikiwa na kupewa fomu ya fidia
namba 69.
"Fomu hii
ilitolewa na maafisa ardhi wakati wa uthamini wa fidia na inayo kumbukumbu namba, mfidiwa atatakiwa
kuonyesha fomu hiyo kama ushahidi" alisema.
Alisema kwa wananchi walioko jirani na bwawa hilo watatakiwa kuhama ndani ya
miezi 6 huku wale wale ambao barabara imepita maeneo yao watatakiwa kuondoka
ndani ya miezi mitatu kupisha ujezi huo.
"Ni lazima
tuanze kutengeneza barabara inayoanzia Ngerengere hadi katika bwawa hilo alafu
ndipo tuanze ujenzi wa bwawa" alisema.
Mbunge wa
jimbo la Morogoro Kusini Inocent
Karogeries aliwataka wananchi hao kuhakikisha fedha hizo wanazitumia kujenga
makazi bora na sio kuzitumia katika matumizi mengine.
Mwenyekiti
wa halimashauri ya wilaya ya Morogoro Kibena Kiongo aliwataka viongozi kutowalazimisha wananchi
hao na kuwachgulia Benk ya kujiunga kwaajili ya zoezi hilo na badala yake
wawaache wenyewe wafanye maamuzi.
Naye
mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Morogoro Yona Maki alisema tayari
viwanja 1000 ( elfu moja vimeshapimwa kwaajili ya makazi ya wananchi hao.
Alisema watu
2600 ndio wanatakiwa kufidiwa katika zoezi hilo kwa upande wa barabra
itakapopita na wale wanaishi jirani na bwawa hilo.
Bwawa la
Kidunda linajengwa kwaajili ya kuchukua maji kutoka katika mto Ruvu kwaajili
ya kusaidia kuwa na uhakika wa maji
katika kipindi chote cha mwaka.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269