Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete akiwasili katika eneo la mradi wa nyumba za
makazi Mkuzo na kukaribishwa na wenyeji wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa
Shirika la Nyumba la Taifa, Bw. David Misonge Shambwe (mwenye tisheti ya
pundamilia).
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili katika eneo la tukio ambako alizindua mradi huo.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete akifunua jiwe la
msingi wakati wa ufunguzi wa nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na
Shirika la Nyumba la Taifa huko Mkuzo wilayani Songea Mjini, mkoani
Ruvuma jana. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la
Taifa, Bw. David Misonge Shambwe na wa pili kushoto ni Waziri wa Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Kajumulo Tibaijuka, kulia ni
Mama Salma Kikwete, Mke wa Rais.
Rais
Jakaya Kikwete na Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Mh. Saidi Mwambungu (kulia),
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi Mh. Profesa Anna Tibaijuka (kushoto)
na Kaimu Mkurugenzi wa shirika la Nyumba NHC Bw. David Shambwe wakikata
utepe kwa pamoja kama ishara ya uzinduzi wa mradi huo.
Kaimu
Mkurugenzi wa shirika la Nyumba NHC Bw David Shambwe akitoa taarifa za
mradi wa huo wa gharama nafuu wa Mkuzo kwa Rais Dr. Jakaya Kikwete.
Mkuu wa
Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Jamii Cha Shirika la Nyumba la
Taifa (National Housing) Susan Omari akitoa maelezo kwa Rais Dkt. Jakaya
Mrisho Kikwete kuhusu mashine za kutengeneza matofali aina ya Hydraform
ambazo zitagawanywa kwenye wilaya zote za Mkoa wa Ruvuma ili kuwezesha
vikundi vilivyoanzishwa vya ujenzi vya vijana kuendelea na mafunzo .
Anayezishuhudia Mashine hizo ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi, Profesa Anna kajumulo Tibaijuka.
Rais
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete, Waziri wa
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Kajumulo Tibaijuka
na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Saidi Mwambungu wakizishuhudia mashine za
kufyatulia matofali aina ya Hydraform ambazo zitagawanywa kwenye wilaya
zote za Mkoa wa Ruvuma ili kuwezesha vikundi vilivyoanzishwa vya ujenzi
vya vijana kuendelea na mafunzo .
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Makazi Mh. Profesa Anna Tibaijuka akizungumza katika
hafla hiyo jana, kushoto kwake ni Waziri wa Ujenzi, Dk John Pombe
Magufuli, wabunge na viongozi mbalimbali wa mkoa huo walioshuhudia tukio
hilo.
Rais
Dr. Jakaya Kikwete akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo, ambapo
aliziagiza halmashauri za miji kuzipa maeneo taasisi mbalimbali za umma
zinazojishughulisha na masuala ya uendelezaji miji ili waweze kupanga
miji vizuri na kuboresha madhari.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akiwasalimia wananchi waliofika kushuhudia
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dk. Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe
mama Salma Kikwete wakiwasalimia wananchi waliofika kushuhudia
Wananchi waliofika kushuhudia tukio la uzinduzi wakiwa wamejipanga kando ya barabara.
Msafara
wa Rais ukiondoka jana katika eneo la tukio baada ya kumaliza ufunguzi
wa nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa
huko Mkuzo wilayani Songea Mjini, mkoani Ruvuma.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete akikagua
mojawapo ya nyumba iliyokuwa ya mfano wakati wa ufunguzi wa nyumba za
gharama nafuu zilizojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa huko Mkuzo
wilayani Songea Mjini, mkoani Ruvuma.
Kikundi cha ngoma na burudani kikiburudisha hadhira iliyofika eneo hilo la Mkuzo kabla ya Rais kufika.
....................................................................................
Rais Kikwete amerejea kauli yake aliyoitoa Kasera, Mkinga Tanga
kwamba Halmashauri zizipatie taasisi zingine zinazojishughulisha na
uendelezaji miliki kama NSSF, PPF, GEPF, PSPF, LAPF na kadhalika maeneo
kwa masharti ili ziweze kujenga.
Rais Kikwete aliambiwa kuwa katika eneo hilo la Mkuzo, shirika
hilo limejenga kiasi cha nyumba 18 za kuuza na zimejengwa kwa gharama ya
sh. milioni 676.
Rais Kikwete pia ameambiwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la
Nyumba la Taifa, Bw. David Misonge Shambwe kuwa nyumba hizo zimejengwa
katika kutekeleza kaulimbiu ya NHC ya "Nyumba yangu, Maisha yangu"
ambayo mpaka sasa inatekelezwa katika mikoa 14. Ujenzi wa nyumba hizo
ulianza Januari mwaka jana na unakamilika mwezi ujao, Agosti, 2014.
Nyumba hizo, ameambiwa Rais Kikwete, kuwa zitauzwa kwa gharama ya
kati ya sh. milioni 33 na 44 bila kodi ya VAT lakini ambayo inaongezeka
na kuwa kati ya milioni 44 na 52 kwa kutegemea ukubwa wa nyumba -
kuanzia ya vyumba viwili hadi nyumba vitatu. Rais Kikwete anaendelea na
ziara yake mkoani humo.
Mkuzo Housing Estate ni mradi wa nyumba 18 zilizopangwa
kwa kuzingatia vigezo vya miji ya kisasa yenye huduma za msingi zikiwemo
Zahanati , shule ya Chekechea , maduka , sehemu za shughuli mbalimbali
za jumuiya, barabara pana inayotoa fursa kwa watembea kwa miguu na
baiskeli kuwa huru vile vile imezingatia nafasi za miundombinu kama vile
mitaro na umeme.
Kila nyumba inajitegemea ikiwa na eneo kubwa kwaajili ya matumizi
binafsi ya wakazi pamoja na eneo la maegesho ya magari hadi matatu.
Mkuzo Housing estate ina nyumba za aina mbili, nyumba za vyumba
vitatuna nyumba za vyumba viwili . Nyumba za vyumba vitatu zin aukubwa
wa mita za mraba 85 kwa zile zenye jiko la nje na mita 70 zenye jiko la
ndani. Huku nyumba ya vyumba viwili ikiwa na mita za mraba 56. Zinauzwa
kati ya Sh 33 milioni bila VAT na 44 milioni.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269