Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete akikata utepe kuzindua maktaba ya shule ya sekondari ya Chalinze mjini Chalinze jana ambayo imejengwa na Kampuni ya Tanga Cement kupitia bidhaa yake ya Simba Cement kwa kushirikiana na taasisi ya Read International kwa gharama ya shilingi milioni 42 za kitanzania katika kuboresha elimu jimboni humo, Mbunge huyo pia ameahidi kujenga jiko katika shule hiyo na kuongeza kompyuta ili wanafunzi wajengewe mzingira mazuri zaidi ya kujisomea lakini pia ameahidi kushughulikia tatizo la wanafunzi 10 ambao wamefauru kwenda kidato cha ano na sita lakini hawakupata nafasi ya kuchaguliwa, hivyo ameueleza uongozi wa shule hiyo pamoja na wazazi kwamba wanafunzi hao lazima watafutiwe nafasi ya kuendelea na shule hata kama itakuwa siyo ndani ya jimbo la Chalinze, "Muhimu wapate nafasi ya kuendelea na elimu yao ya kidato cha tano na sita" Alisema Mh. Ridhiwani Kikwete alimuomba mwenyekiti wa bodi ya shule hiyo Bw. Mbwana Madeni amkabidhi majina ya wanafunzi wote kumi ili yaanze kufanyiwa kazi mara moja.
Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh Ridhiwani Kikweteakipata maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa bodi ya shule ya sekondari Chalinze Bw. Mbwana Madeni kabla ya kuzindua rasmi maktaba ya shule hiyo, Katikati ni Emma Lyu kutoka taasisi ya Read International na kushoto ni Raquel Araya kutoka Taasisi ya Read International pia.
Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh Ridhiwani Kikwete akionyeshwa vitabu mbalimbali vilivyopo katika maktaba ya shule ya sekondari ya Chalinze na Najma Juma kutoka Chuo Kikuuu cha Dar es salaam UDSM ambaye anafanya kazi za kujitolea katika taasisi ya Read Internional.
Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh Ridhiwani Kikweteakiangalia kitabu wakati akikagua maktaba hiyo kulia kwake ni Najma Juma wa Read International.
Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh Ridhiwani Kikweteakiweka alama za kiganja chake kama kumbukumbu wakati alipozindua maktaba hiyo jana kwenye shule ya sekondari ya Chalinze.
Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh Ridhiwani Kikwete akifurahia jambo wakati Mwenyekiti wa bodi ya shule ya sekondari Chalinze Bw. Mbwana Madeni alipokuwa akisoma risala yake mbele ya mbunge huyo, kutoka kulia ni Raquel Araya kutoa taasisi ya Read International na mkuu wa ituo cha polisi cha Chalinze Afande J.S Magomi.
Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh Ridhiwani Kikwetea akizungumza na wanafunzi wa sule ya sekondari ya Chalinze pamoja na walimu mara baada ya kuzindua maktaba katika shule hiyo jana kushoto ni Mbwana Madeni mwenyekiti wa bodi ya shule, na kutoka kulia ni Raquel Araya kutoka Read International na mkuu wa ituo cha polisi cha Chalinze Afande J.S Magomi.
Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh Ridhiwani Kikwetea akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuzindua maktaba hiyo kushoto ni mdau wa masuala ya habari Dk Fadhil Kabujanta wa Fadhaget Sanitarium Clinic ya Mbezi Africana jijini dar es salaam.
Meneja masoko wa Simba Cement Yasin Hussein akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa Maktaba ya shule hiyo iliyojengwa na Kampuni hiyo gharama yake ikiwa ni shilingi milioni 42 za kitanzania. PICHA NA FULLSHANGWE BLOG
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269