Breaking News

Your Ad Spot

Aug 24, 2014

MTEMVU AONGOZA SEMINA KUTATHMINI UTEKELEZAJI WA ILANI JIMBONI MWAKE LEO

 Mbunge wa Temeke ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Abbas Mtemvu akiendesha kikao cha Wenyeviti wa mitaa katika jimbo la Temeke, leo kwenye Ukumbi wa Manispaa ya Temeke, Dar es Salaam, kwa lengo la kufanya tathmini ya utekelezaji wa Ilani ya CCM katika jimbo hilo. Katika kikao hicho walihudhuria pia viongozi wa Chama wa ngazi za juu katika mitaa hiyo. Kushoto ni Katibu wa Jimbo la Temeke Kasim Kiame na kulia ni Mwenyekiti wa jimbo Ahmad Mnamala.
 Mtemvu akitoa ufafanuzi kuhusu hoja mbalimbali zilizotolewa na wajumbe kwenye kikao hicho. Kushoto ni Mwenyekiti wa Wenyeviti wa Mitaa, Athuman Mohamed na wapili ni Katibu wa Jimbo la Temeke Kasim Kiame.
Mwenyekiti wa Wenyeviti wa mitaa, Athuman Mohamed akizungumza kwenye kikao hicho.
 Naibu Meya wa Manispaa ya Temeke, Juma Mkenga (kulia) akizungumza wakati wa kikao hicho cha kutathmini na kujadili utekelezaji wa ilani ya CCM jimbo la Temeke.
 Wajumbe wakiwa ukumbini
 Wajumbe wakiwa ukumbini kwenye kikao hicho
Baadhi ya wajumbe wakinyoosha mikono kuomba kuchangia hoja. Picha zote na Bashir Nkoromo wa theNkoromo Blog.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages