NA BASHIR NKOROMO
CHAMA
Cha Mapinduzi (CCM) kimepokea kwa furaha Chama cha Frelimo kuibuka na
ushindi katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 15, mwaka huu.
Katika
uchaguzi huo, aliyekuwa mgombea kwa tiketi ya Frelimo, Filipe Nyusi
ameibuka kidedea na sasa ndiye Rais Mteule wa Msumbiji ambaye baada ya
kuapishwa atashika mikoba itaakayoachwa na Rais anayemaliza muda wake,
Armando Gwebuza.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo, katika ukumbi wa Sekretarieti, Ofisi Ndogo
ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam. Katibu wa NEC,
Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye (Pichani), amesema, CCM imepokea ushindi
huo kwa furaha kubwa kutokana na undugu wa damu uliopo baina yake na
Frelimo kwa mikaka mingi.
"Chama
Cha Mapinduzi kilifuatilia kwa karibu kwa kuwa CCM na Chama cha Frelimo
ni vyama ndugu vyenye historia moja na ya pamoja ya Ukombozi Kusini mwa
Afrika. Historia hiyo ndiyo iliyomfanya Rais Mteule wa nchi hiyo Ndugu
Filipe Nyusi mara baada ya kuteuliwa kwake na Frelimo kugombea Urais,
nchi ya kwanza kuitembelea kuwa Tanzania", alisema Nape na kuongeza;
"Ikumbukwe
kwamba huyu si mgeni hapa Tanzania. Kama wanaharakati wengine wa
ukombozi, Ndugu Nyusi aliishi Tanzania, anaongea vizuri Kiswahili na
anaichukulia Tanzania ni nyumbani".
Alisema
kwa mnasaba huo, Chama Cha Mapinduzi na Watanzania kwa ujumla wana kila
sababu ya kushangilia ushindi walioupata ndugu zao wa Frelimo, kwa kuwa
ushindi huo ni wa wote.
"Tunampongeza
sana Rais Mteule Filipe Nyusi kwa kupeperusha vema bendera ya Frelimo.
Matokeo ya Uchaguzi yamedhihirisha imani kubwa waliyonayo wana-Msumbiji
kwa Frelimo na kwa Rais Mteule Filipe Nyusi", alisema Nape.
Nape
amesema CCM ina imani kwamba chini ya uongozi imara wa Mwenyekiti wake
Dk. Jakaya Kikwete, na Rais Mteule Filipe Nyusi, uhusiano kati ya vyama
vya CCM na Frelimo utaimarika na kustawi.
Kadhalika
Chama Cha Mapinduzi kimempongeza Armando Guebuza kwa kuiongoza Frelimo
na Taifa lake vema na kukamilisha uongozi wake kwa mafanikio makubwa.
"Anapoanza
kipindi hiki cha uongozi wa Taifa lake, sisi wana-CCM tunamtakia Ndugu
Nyusi afya njema, busara, maarifa na uongozi uliotukuka", alisema Nape.
Alisema,
CCM itasimama pamoja na Frelimo katika kuendeleza urithi ulioachwa na
waasisi wa vyama vyao, Mwalimu Julius Nyerere na Samora Machel.
Your Ad Spot
Oct 31, 2014
Home
Unlabelled
CCM YAPOKEA KWA FURAHA FRELIMO KUIBUKA ,MSHINDI KATIKA UCHAGUZI MKUU WA MSUMBUJI
CCM YAPOKEA KWA FURAHA FRELIMO KUIBUKA ,MSHINDI KATIKA UCHAGUZI MKUU WA MSUMBUJI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269