Breaking News

Your Ad Spot

Oct 2, 2014

ZIARA YA TANGA, YAMFIKISHA KINANA PANGANI, KIGOGO WA CUF AREJEA CCM

Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman  Kinana akichimba mtaro wa kulaza bomba la majini wakati akizindua mradi wa maji Mkalamo, Pangani leo Oktoba 2, 2014, akiwa katika ziara kukagua na kuhimiza utekelezaji wa ilani ya CCM katika mkoa wa Tanaga.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikinga maji wakati wa kuzindua mradi wa maji wa kata ya Mkalamo wilaya ya Pangani mkoani Tanga.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimtwisha dumu la maji Mariam Hemedi baada ya kuzindua mradi wa maji wa kata ya Mkalamo
Wananchi wakichota maji baada ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kuzindua mradi wa maji Kijiji cha Mlakamo, Pangani, leo, Oktoba 2, 2014, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM katika mkoa wa Tanaga.
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akiondoka na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kwenye  eneo la tukio baada ya kuzindua mradi wa maji, Mkalamo, Pangani. watatu kulia ni Mbunge wa Pangani, Saleh Pamba
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki ufyatuaji matofali, ujenzi wa Ofisi ya CCM Kata ya Mkwaja, Pangani, Tanga.

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akibeba tofali baada ya kushiriki ufyatuaji matofali kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi ya CCM Kata ya Mkwaja, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na kukagua uhai wa Chama katika wilaya ya Pangani mkoa wa Tanga
Kinamama wa Pangani wakimwimbia Kinana  baada ya kushiriki kumenya  na kuchambua Popoo na wananchi wa Kijiji cha Mseko, Pangani mkoa wa Tanga.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki kumenya na kuchambua Popoo katika Kijiji cha Mseko, Pangani, leo Oktoba 2, 2014, akiwa katika ziara kukagua na kuhimiza utekelezaji wa ilani ya CCM katika mkoa wa Tanga.
Popoo za Pangani mkoa wa Tanga ndizo hizi. zao hili ndizo hutumika kutengeza tambuu kwa kuchangaywa na vitu vingine, tambuu hizo hutumiwa zaidi na watu wenye asili ya Kiasia.
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akizungumzana wananchi kwenye uzinduzi wa Ofisi ya CCM  tawi la Mseko, akiwa katika ziara ya kukagua uhai wa chama na kukagua na kuhimza utekelezaji wa ilani ya CCM katika wilaya ya Pangani mkoa wa Tanaga, leo Oktoba 2, 2014.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki kuweka dirisha wakati akishiriki ujenzi wa Ofisi ya CCM Kata ya Mseko Pangani, akiwa katika ziara ya kukagua uhai wa Chama na kukagua na kuhimza utekelezaji wa Ilani ya CCM katika wilaya ya pangani mkoa wa Tanga.  Kushoto ni Mbunge wa Pangani Saleh Pamba.
Mkazi wa Kijiji cha Mwera, Pangani, Gabriel Saifee, akimshangilia Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana wakati wa mkutano wa hadhara  uliofanyika katika kijiji hicho, Pangani mkoa wa Tanga, leo Oktoba 2, 2014.
Wananchi baadhi wakiwa na biashara zao kwenye mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana katika Kijiji cha Mwera, Pangani, Tanga.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye  akihutubia katika mkutano wa Kinana uliofanyika leo, Oktoba 2, 2014, kwenye Uwanja wa Kijiji cha Mwera, pangani Tanga.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia mkutano wa hadhara aliofanya kwenye Uwanja wa Mwera, Pangani, leo Oktoba 2, 2014, akiwa katika ziara ya kukagua na kuhimiza utekelezaji wa ilani ya CCM katika mkoa wa Tanga.
Mbunge wa Pangani, Salehe Pamba akizungumza na wapigakura wa jimbo hilo, katika mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana uliofanyika kwenye Uwanja wa mpira wa  Mwera, Pangani Tanga.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipokea kadi ya CUF kutoka kwa aliyekuwa mwanachama wa chama hich, Ramadhani Rashid, baada ya kutangaza kuhama chama hicho na kujiunga na CCM katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo, Oktoba 2, 2014 kwenye Uwanja wa Mwera, pangani mkoa wa Tanga. Kushoto ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.
Wananchi wenye heshima, rika na umri mbalimbali wakiwa wamehudhuria kwenye mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana uliofanyika leo Oktoba 2, 2014 kwenye Uwanja wa Mwera Pangani mkoa wa Tanga.

  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahma Kinana akiwapongeza wachezaji wa timu ya soka ya Mwera baada ya timu hiyokuibuka mshindi kwa kuitungua mabao 5-4 timu ya Usongo, zote za Kijiji cha Mwera katika mechi ya kuwania mbuzi iliyochezwa baina ya timu hizo kwenye Uwanja wa Mwera,  kumpokea Kinana Pangani.
Baadhi ya wachezaji wa timu ya soka ya Mwera wakishangilia zawadi ya mbuzi, waliyokabidhiwa na Kinana baada ya kuitungua mabao 5-4 timu ya Usongo, zote za Kijiji cha Mwera katika mechi ya kumpokea Kinana Pangani. Picha zote na Bashir Nkoromo-theNkoromo Blog

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages