Breaking News

Your Ad Spot

Nov 18, 2014

FILAMU MPYA YA 990 WAMEKUFA IPO MBIONI KUZINDULIWA, WADAU WAOMBWA KUCHANGIA

Hii  ndio  filamu mpya ya 990  wamekufa  inayotarajiwa  kuzinduliwa  hivi karibuni na wasanii wa Miale  sanaa Group wa Iringa
 Mkurugenzi mtendaji wa  Miale  sanaa Group Bw  Nurdin Khamis  kushoto wa kwanza akiwa na   baadhi ya  wasanii  wanaounda kundi hilo 
 Mkurugenzi mtendaji wa  Miale  sanaa Group Bw  Nurdin Khamis akihojiwa
Na  MatukiodaimaBlog

WASANII  wasanii wa   Miaele sanaa Group  wa mjini Iringa mkoani Iringa waanza kutembeza bakuli kuomba  kuchangia  kiasi cha Tsh milioni 3 kwa ajili ya kukamilisha uzinduzi  wa  filamu yao mpya  ya 990 wamekufa .
Akizungumza na mtandao  wa matukiodaima.co.tz   mkurugenzi  mtendaji  wa  kundi  hilo Nurdini Khamis alisema  kuwa   kundi hilo  limeendelea  kufanya vema katika  tasnia ya  filamu  nchini  kutokana na  wasanii  wake  kuifanya  kazi hiyo kwa  kutumia vipaji halisi vya  kuzaliwa na hivyo  kuwa  tofauti na  wasanii  wengine  ambao  wamekuwa  wakiifanya kazi  hiyo kwa  kutegemea elimu  ya  vyuo  vya  sanaa.

Alisema  kuwa kuanzishwa kwa  kundi hilo ni  jitihada  zake  binafsi  baada ya  kuona  mkoa wa Iringa una wasanii wenye uwezo wa  kuigiza  ila hakuna  sehemu ya kuonyesha  vipaji vyao na ndipo alipoanzisha  kundi  hilo mwaka 2009 kwa  kuwa na  wasanii 30  kabla ya  kufanyiwa mchujo .

Khamis  alisema  kuwa  mara  baada ya mazoezi  makali  zaidi  wale ambao  walifanyiwa mchujo  waliweza  kuonyesha  uwezo mkubwa katika  uigizaji na  hivyo kulazimika  kutoa kazi yao ya kwanza  iliyokwenda kwa  jina la  Zero Done kwa  kuwashirikisha  wasanii  wakubwa  nchini kama  Senga , Mwamba , Mzee Pembe , Patcho ,Halima Madiwa , Rado  na  wengine  wengi  wenye majina makubwa  kazi ambayo ilisambazwa  nchi nzima na  kuonyesha  kupendwa  zaidi.

Aidha  alisema  kutoka na ukata wa  fedha  wameendelea  kufanya kazi  hiyo kwa  kusua  sua  japo kwa  sasa  wanataraji  kuibuka na filamu kali kuliko ya 990  wamekufa ambayo  inategemewa  kuzinduliwa  wakati  wowote  kuanzia  sasa mara  baada ya maandalizi  kukamilika.

Mkurugenzi  huyo alisema  kuwa  kutokanana na uwezo mdogo  wa kipato na aina ya  wasanii  wanaounda kundi  hilo kutokuwa na kazi za kufanya kundi  hilo  limeendelea  kuwa  tegemezi zaidi kwa  kufanya kazi kwa migongo ya  wafadhili mbali mbali na kuwa  hata  filamu  hiyo  iliyopo jikoni  inategemea  kuzinduliwa kwa ufadhili wa    kamanda wa UVCCM mkoa  Salim Asas , Jackson Kiswaga ambae ni mkazi wa Iringa na mdau wa sanaa katika  mkoa wa Iringa aliyechangia kiasi cha Tsh 500,000

Pamoja na  kuwashukuru  wadau mbali mbali kwa  kuendelea  kujitolea kusaidia  ukuaji wa tasnia ya sanaa katika  mkoa  wa Iringa bado  alisema  kuwa ni mategemeo yao  kuwa wadau hao wataendelea  kutoa ushirikiano  zaidi kwao  ili  kufanikisha  kuutangaza  zaidi mkoa wa Iringa  kisanaa kutokana na  uwezo mkubwa  wa wasanii  wanaounda  kundi  hilo.

Kwani  alisema  mipango ya mbeleni  kwa  kupitia  kundi hilo kuanzisha utaratibu  wa kutengeneza  filamu  za kuelimisha  jamii  juu ya masuala mbali mbali ya kimaendeleo  katika  mkoa wa Iringa na Taifa  kwa  ujumla ikiwa ni  pamoja na kutoa  elimu ya kulinda hifadhi  zetu kutoingiliwa na majangili .

Hivyo  aliomba  wale  wote  wenye mapenzi ya  dhati na kundi hilo  kujitokeza  kuchangia  chochote kwa kupitia  huduma ya M- Pesa  kwa namba  0757 698 582 kwa madai kuwa  bila  kusaidiwa na  wadau  mbali mbali  uwezo  wao ni mdogo  zaidi kiuchumi ila  kisanaa wapo  juu ukilinganisha na makundi mengine makubwa  nchini.

" Uwezo wa  kucheza  filamu  zenye ubora  tunao na ndio maana vituo  mbali mbali vikubwa vya runinga  ikiwemo  Zuku swahili  wamekuwa wakirusha kazi  zetu baada ya  kuona ni bora zaidi"

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages