Breaking News

Your Ad Spot

Nov 18, 2014

KINANA AMMWAGIA SIFA LUKUKI MBUNGE MTANDA WA JIMBO LA MCHINGA


 Kikundi cha Kwaya kikitumbuiza  wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji uliofanywa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, katika Kijiji cha Mipingo , Kata ya Namkongo, wakati wa ziara yake katika Jimbo la Mchinga, Lindi Vijijini, ya kuimarisha uhai wa chama na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2010.

 Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Kata ya Milola, Jimbo la Mchinga, Lindi leo, ambapo aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa Desemba 14, mwaka huu. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akilakiwa alipowasili Jimbo la Mchinga, katika Kijiji cha KJitomanga, Kata ya Mkwajuini kukagua ujenzi wa ghala la kuhifadhia nafaka.

 Wananchi wakisikilza wakati Kinana akihutubia alipokagua na kushiriki ujenzi wa ghala la kuhifadhia nafaka na mazao mengine katika Kata ya Mkwajuni

 Wananchi wakishangilia huku wakiwa na matawi wakati wa mapokezi ya Kinana na msafara wake katika Kijiji cha Mipingo, Jimbo la Mchinga, ambapo alizindua mradi wa maji na kukabidhi simenti ya kusafakia soko

 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akihutubia wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi wa maji uliogharimu sh. mil. 166 katika Kijiji cha Mipingo  Namkongo, Jimbo la Mchinga.

 Kinana akikabidhi mifuko ya simenti kwa ajili ya kujengea sakafu ya Soko la Mipingo, Namkongo, Jimbo la Mchinga, Lindi

 Kinana akimtwisha ndoo ya maji mmoja wa akina mama baada ya kuzindua mradi wa maji katika Kijiji cha Mipingo, Namkongo

 Kinana akikagua soko la Mipingo, Kata ya Namkongo, Jimbo la Mchinga

 Kinana akipata maelezo kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Mchinga kuhusu mradi wa maji wa Kijiji cha Mipingo, Kata ya Namkongo

 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akimsikiliza  Mgombea Mteule wa CCM wa nafasi ya Uenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kilangala, Hamid Namponda ambaye awali alikuwa mwanachama wa CUF na sasa amehamia CCM

Kinana akikabidhi baiskeli kwa Seleman Mgunde kwa ajili ya kazi za chamaM la  katika Tawi la CCM Mkumbila, Jimbo la Mchinga, Lindi

 Kinana akisaidia ujenzi wa Zahanati ya Mchinga 11 wakati wa ziara yake Jimbo la Mchinga, Lindi leo

 Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Lindi, Ally Mtopa akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Kata ya Milola

 Mjumbe wa NEC Taifa, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mtama na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Kata ya Milola, Jimbo la Mchinga, Lindi

Vijana waliofuzu mafunzo ya uendeshaji wa Bodaboda wakiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Mbunge wa Jimbo la Mchinga, Said Mtanda baada ya kukabidhiwa vyeti vyao katika mkutano wa hdhara katika Kata ya Milola, Jimbo la Mchinga, Lindi

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages