Henry Kapinga, mmiliki wa KAPINGAZ Blog
Leo
tarehe 08/12 ndio siku ambayo ukurasa wa historia ya maisha yangu
ulifunguliwa rasmi, ni siku ambayo nilizaliwa, napenda kuchukua nafasi
hii kumshukuru mwenyezi Mungu kwa kuniweka mpaka leo na vilevile
kuwashukuru wazazi wangu kwa kunilea katika maisha yangu ya utotoni
mpaka nilipoanza kujitegemea.
Napenda
kuchukua fursa hii pia kuwashukuru wale wote ambao kwa namna moja au
nyingine wameshiriki kunisapoti kwa mambo mbalimbali ili mradi nifikie
pale ambapo waliamini ni sehemu bora zaidi katika maisha yangu, vilevile
napenda kumpongeza Mama yangu mdogo Mama Kasulus Kapinga ambaye na yeye
tumezaliwa tarehe moja na mimi, nasema Hongera sana.
Ntakuwa
mnyimi wa fadhila bila kuwashukuru MABLOGGER wenzangu kwa ushirikiano
tulionao katika kuiendeleza tasnia hii ambayo kwetu Tanzania bado ni
changa.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269