Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho
Kikwete (pichani, akiwa ofisini, Ikulu) amemteua Mkuu Mpya mmoja wa Mkoa na kuwahamisha vituo vya kazi
wengine sita kuanzia jana, Jumamosi, Desemba 6, 2014.
Taarifa
iliyotolewa leo, Jumapili, Desemba 7, 2014 na Katibu Mkuu Kiongozi
(KMK), Balozi Ombeni Sefue mjini Dar es Salaam inasema kuwa Rais
amemteua Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Mkoa wa Arusha, Ndugu Daudi Felix
Ntibenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
Ndugu Ntibenda ataapishwa kesho, Jumatatu, Desemba 8, 2014, saa nne asubuhi, Ikulu, Dar Es Salaam.
Taarifa
hiyo inasema kuwa wakuu waliohamishwa vituo vya kazi ni Mheshimiwa
Elaston Mbwilo anayehamishwa kutoka Mkoa wa Manyara kwenda Mkoa wa
Simiyu ambako anachukua nafasi ya Mheshimiwa Paschal Mabiti aliyepewa
likizo ya ugonjwa, Mheshimiwa Joel Nkanga Bendera aliyehamishwa Mkoa wa
Manyara kutoka Mkoa wa Morogoro na Mheshimiwa Dkt. Rajabu M Rutengwe
anayehamishwa Mkoa wa Morogoro kutoka Mkoa wa Tanga.
Wengine ni
Mheshimiwa Magalula Saidi Magalula anayehamishiwa Mkoa wa Tanga kutoka
Mkoa wa Lindi, Mheshimiwa Mwantumu Bakari Mahiza anayehamishiwa Mkoa wa
Lindi kutoka Mkoa wa Pwani na Mheshimiwa Mhandisi Evarist B. Ndiliko
anayehamishiwa Mkoa wa Pwani kutoka Mkoa wa Arusha. Wakuu wengine wa mikoa wanaendelea kubakia katika vituo vyao vya sasa vya kazi.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu Dar es Salaam.
6 Desemba,2014
Your Ad Spot
Dec 7, 2014
Home
Unlabelled
RAIS KIKWETE APANGUA BAADHI YA WAKUU WA MIKOA, ATEUA MPYA MMOJA
RAIS KIKWETE APANGUA BAADHI YA WAKUU WA MIKOA, ATEUA MPYA MMOJA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269