Breaking News

Your Ad Spot

Dec 5, 2014

WAFANYAKAZI WA TBL WALIOPIMA UKIMWI WAZAWADIWA


Mgeni rasmi Ofisa Uendeshaji, Rasirimali watu wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Collins Constantine, akishishirikiana na wafanyakazi wenzake wa TBL kuwasha mishumaa kuwakumbuka wenzao waliopoteza maisha kwa ugonjwa wa Ukimwi.

  Mgeni Ofisa Uendeshaji, Rasirimali watu wa Kampuni ya Bia Tanzania
(TBL), Collins Constantine akikabidhi zawadi ya jiko la gesi kwa
Christopher Mchome, baada ya kushinda bahati nasibu ya wafanyakazi
waliopima afya zao, wakati wa maadhimisho ya siku ya Ukimwi, Dar es
Salaam juzi.

 Mchome akisaidiwa na wenzake kubeba jiko baada ya kushinda bahati nasibu ya wafanyakazi wa TBL.

 Wasanii wakitoa burudani ya michezo mbalimbali wakati wa maadhimisho hayo kwa wafanyakazi wa TBL.



 Wafanyakazi wa TBL wakisubiri kwa shauku kubwa zawadi zilizotolewa na kampuni hiyo ili zichezeshwe bahati nasibu kwa wafanyakazi waliopima afya zao kwa hiari.

 Wakiwa na shauku ya kupata zawadi, wafanyakazi wa TBL wakipata kinywaji huku wakisubiri bahati nasibu iliyoandaliwa na kampuni hiyo, wakati wa maadhimisho ya siku ya Ukimwi.



 Mfanyakazi wa Kampuni ya Bia Tanzania TBL, Joel Saganya akiwa mwenye furaha baada ya kushinda gogoro.

 Wasanii wakionyesha umahili wao wa kucheza Sarakasi

Sarakasi ilikuwa moja ya michezo iliyowavutia wafanyakazi wa TBL

Wakiwa na shauku ya kupata zawadi, wafanyakazi wa TBL wakipata kinywaji huku wakisubiri bahati nasibu iliyoandaliwa na kampuni hiyo, wakati wa maadhimisho ya siku ya Ukimwi.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages