Breaking News

Your Ad Spot

Feb 16, 2015

Baada ya Ivory Coast kutwaa AFCON, haya ndiyo maamuzi ya Kolo Toure…

koloMlinzi wa timu ya Liverpool Kolo Toure amethibitisha kuwa amestaafu kucheza soka la kimataifa  wakati akiwa na timu yake ya Ivory Coast iliyotwaa kombe la Mataifa ya Afrika AFCON.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 aliweka wazi kuwa mchezo wake wa mwisho kuonekana uwanjani ulikuwa dhidi ya timu ya Equatorial Guinea.
tou
Kolo anasema anaipenda nchi yake na hasa anachokipenda zaidi maishani mwake ni Kandanda,lakini amesisitiza kuwa huu ni wakati wake wa kusitisha kuendelea kucheza.
Najisikia vibaya sana kuwafahamisha kuwa ni wakati wangu kuwaaga,Lengo langu lilikuwa kushinda katika michuano ya kombe la mataifa ya Africa, na nakubali ulikuwa ni uamuzi mgumu kutangaza“:- Kolo Toure.
Toure amekuwa kiungo muhimu sana katika kuutengeneza ushindi wa timu na taifa lake katika kipindi cha miaka ya 2006, 2010 and 2014 akiwa na kikosi cha timu yake ya taifa katika michuano ya kombe la dunia.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages