Na Francis Godwin, Njombe MBUNGE
wa jimbo la Ludewa, Deo Filikunjombe (pichani), amewavaa Mawaziri
walioteuliwa na Rais Jakaya Kikwete kutoka Mkoa wa Njombe kwa kushindwa
kusaidia ukuaji wa mkoa huo, na badala yake kuwa mawaziri wa kulalamika
tu. Mbunge Filikunjombe aliwavaa Mawaziri hao leo, baada ya Mkuu
wa Mkoa wa Njombe Dk. Rehema Nchimbi kuwapa nafasi Mawaziri na Mbunge
huyo kama wajumbe wa juu wa kikoa cha kamati ya ushauri ya mkoa (RCC),
ili kuchangia juu ya namna ambavyo Mkoa wa Njombe unaweza kupata kiasi
cha Tsh zaidi ya bilioni 158.6 kwa ajili ya bajeti ya mwaka wa fedha
2015/2016. Wakati mawaziri wawili akiwemo Waziri wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa Rais Dr Binilith Mahenge na Naibu Waziri wa Maendeleo ya
Jamii, Jinsia na Watoto,Pindi Chana wakitaka watumishi wa umma
kuwajibika vema katika ukusanyaji wa mapato. Waziri Dk Pindi ambaye
ni Mbunge wa viti maalum mkoa wa Njombe akichangia alisema ni suala la
Halmashauri kujitathimini kwani ni jambo na kujiuliza kwa halmashauri
kujipangia makusanyo na kushindwa kutimiza malengo yake .
Huku
waziri Dk. Mahenge ambae ni mbunge wa jimbo la Makete akiutaka mkoa
kuwabana wakuu wa idara kuwa na matumizi mazuri ya fedha kwa kuwa na
nidhamu ya matumizi ya fedha za umma badala ya kuwa na matumizi mabaya
pia kuangalia uwezekano wa kutupunga watumishi wasio na tija katika
Halmashauri .
Blioni 9 zinategemewa kukusanywa katika mkoa wa
Njombe kwa mwaka wa fedha 2015/2016 huku mkoa huo ukiomba maalum ya
kuhidhinishiwa kiasi cha zaidi ya Tsh bilioni 158.6 kwa ajili ya
uendeshaji wa mkoa kwa maana ya kulipa mishahara ya watumishi ,miradi ya
kimaendeleo na matumizi mengine. Kwa upande wake mbunge wa Ludewa Bw
Filikunjombe akichangia juu ya mkakati huo wa uopatikanaji wa kiasi
hicho cha fedha za uendeshaji wa mkoa alisema kuwa kwa upande wake
asingependa kuchangia suala hilo kwani wapo mawaziri katika mkoa wa
Njombe ambao ndio wapo jikoni hivyo ni matumaini yake kusikia majibu yao
badala ya kuishia kulalamika. Mbunge Filikunjombe akichangia katika kikao cha RCC Njombe. Mjumbe wa kikao cha RCC alikuwa akichangia jinsi ambavyo Serikali Kuu inavyokwamisha maendeleo wilayani.
"Kweli mimi mheshimiwa mwenyekiti
kunitaka niseme hapa ni kunionea kwani humu ndani katika kikao chetu
tunao vijana wetu ambao ni mawaziri sasa ni vema wao kusema zaidi na sio
kuishia kulalamika....maoni yangu binafsi haya ni maoni yangu binafsi
sana .....mimi ningependa sana kila mmoja kutimiza wajibu wake serikali
itimize wajibu wake wabunge na watendaji pia hivyo hivyo.... kuna shida
hapa tunapanga mambo tunawapangia hadi wahisani halafu baadae tunaanza
kulalamika". Mbunge Filikunjombe aliwataka watendaji serikali kuacha
kuwa walalamikaji na badala yake kila mmoja kutimiza wajibu wake kwa
pale walipo.
Alisema kuwa ilipendeza mawaziri hao ambao ndio
serikali kuu kuzipongeza Halmashauri za mkoa wa Njombe kwa kufanikisha
kukusanya mapato kwa asilimia 40 badala ya kutoa majibu ya kulalamika
huku Halmashauri hizo zikiendelea kuidai serikali kuu pesa zao za ushuru
wa mazao zaidi ya mamilioni bila kulipa kwa wakati.
Hivyo alisema kwa kuwa wapo vijana ndani ya serikali kuu ni ukombozi wa Halmashauri za mkoa wa Njombe zinazoidai Serikali Kuu. katika
hatua nyingine mbunge Filikunjombe alieleza kusikitishwa baadhi ya watu
wanaotaka nafasi za uongozi na biashara kwa kutumia viungo vya watu
wenye ulemavu wa ngozi (albino) na kumtaka mkuu wa mkoa wa Njombe
kuandika barua katika taasisi zote za dini na vyama vya siasa ili
kusaidia kukemea suala hilo kabla ya kuingia mkoani hapo.
Alisema
kuwa imekuwa ikisikika katika mikoa mingine mauaji na ukatili wa
kutisha japo katika mkoa wa Njombe suala hilo bado hivyo ni vema
kulithibiti mapema .
Wakati waziri Dr Pindi akiungana na kupinga
ukatili wa adhabu ya viboko zaidi ya vitatu kwa wanafunzi nchini pamoja
na kukemea tabia ya baadhi ya wazazi wanaowafundisha watoto wao wa kike
masuala ya uzazi wa mpango kuwa suala hili halina budi kukomeshwa mara
moja.
Hata hivyo mkuu huyo wa mkoa Dr Nchimbi alikubaliana na
ushauri wa Filikunjombe wa kuandika barua kwa taasisi mbali mbali
zikiwemo za dini ili kusaidia kutoa elimu juu ya ukatili mkoani Njombe. wakati
huo huo mkuu huyo wa mkoa wa Njombe Dk. Nchimbi ameagiza wanafunzi wa
shule za msingi katika kukabiliana na hali ya baridi mkoani humo kuanza
kuvaa sare ya suruali badala ya kaptula kama ilivyoagizwa na wizara ya
elimu na mafunzo ya ufundi. Alisema kuwa kutokana na hali ya hewa ya
baridi kali mkoa wa Njombe ni vema viongozi mkoani hapa kuangalia
uwezekana na kufanya mabadiliko ya sare hizo za wanafunzi ili kuvaa
suruali. Alisema kuwa hali ya hewa ya mkoa wa Njombe ni hali ya
baridi kali hivyo kuna haja ya wanafunzi hao kulinda kiafya zaidi kwa
kubadilishiwa sare hizo ili kuvaa suruali kwa ajili ya kujisitili na
baridi kali. "Ndugu wajumbe mkoa wetu ni mkoa wenye baridi kali hivyo
kuendelea kuwaacha watoto wetu kutumia sare hizi za kaptula ni kuwatesa
zaidi ......naona si vibaya kubadili sare na wizara ya elimu na mafunzo
ya ufundi kuelezwa sababu hii mbona wanaume wa Njombe kutokana na
baridi hii wanavaa suruali tena wengine wanavaa mbili zaidi sasa iweje
watoto wetu kuendelea kuteseka na baridi"alisema
Katika hatua
nyingine mkuu huyo wa mkoa alitaka viongozi wa mkoa wa Njombe kuwa na
jibu moja kwa swali la ujenzi wa maabara na uhaba wa madawati kwa kila
wanapoulizwa waseme wamekamilisha ujenzi huo wa maabara mbali ya kuwa
wamekarabati vyumba vya madarasa yaliyokuwepo.
" Naomba tuwekane sawa hapa kuna
vijimaneno maneno vimeanza kusikika kuwa hatujakamilisha ujenzi wa
maabara ukweli sisi tumetumia mbinu zetu kukamilisha maabara kama
tumegeuza vyumba vya madarasa hiyo ni mbinu yetu wao walitaka maabara na
maabara zote zipo na sisi hatuna upungufu wa vyumba vya madarasa wala
maabara"
Wakati huo huo serikali ya mkoa wa Njombe imewataka
viongozi wanaohusika na migao ya fedha za uondeshaji wa mikoa kuutazama
mkoa wa Njombe kwa jicho la tatu ili mgao wake uwe mkubwa zaidi kama
njia ya kuuwezesha mkoa huo kusonga mbele mbele kimaendeleo.
Mkuu
wa mkoa wa Njombe Dk. Nchimbi alisema kimsingi mtoto ndie anayepata
mahitaji bora ili apate kukua hivyo mkoa wa Njombe wenye utajiri mkubwa
wa chuma na makaa ya mawe unahitaji kutengewa bajeti kubwa zaidi ili
kuweza kupita hatua na kuweza kuwa mkoa wa kiuchumi kwa Taifa.
|
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269