Waziri wa Afrika Mashariki Mhe.
Harrison Mwakyembe ambaye alikua mwenyekiti wa mkutano wa kujiandaa
kutiliana saini makubaliano ya biashara na uwekezaji wa nchi za Afrika
Mashariki na Marekani. Utiliani saini huo utafanyika siku ya Alhamisi
Februari 26, 2015 katika Ofisi za Wizara ya Biashara Marekani, kulia ni
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Richard Sezibera
kutoka Burundi.
Ujumbe wa Tanzania
Ujumbe wa Burundi
Ujumbe wa Kenya
Balozi wa Tanzania nchini
Martekani akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya
Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Richard Sezibera kutoka Burundi.
……………………………………………………………
Mkutano
uliowakutanisha Mawaziri wa nchi tano za Afrika Mashariki wakiwemo
Mabalozi wa nchini zao nchini Marekani ulifanyika Februari 25, 2015
katika Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani, mkutano huo uliohusiana na
maandalizi ya kutiliana saini ya makubaliano ya ushirikiano wa
kibiashara na uwekezaji kati ya nchi ya Marekani na nchi za Afrika
Mashariki ambazo ni Burundi, Rwanda, Uganda, Kenya na Tanzania.
Mkutano huo
uliongozwa na mwenyekiti wake Mhe. Harrison Mwakyembe Waziri wa Tanzania
katika bunge la Afrika Mashariki pamoja na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya
Afrika Mashariki Balozi Dkt. Richard Sezibera kutoka Burundi.
Washiriki wengine
kwenye mkutano huo kutoka Tanzania walikua ni Waziri wa Viwanda na
Biashara wa Tanzania Mhe. Dkt. Abdallah Kigoda, Waziri wa Usafirishaji
Mhe. Samwel Sitta, Maria Bilia Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na
Biashara, Amantius Msole, Naibu Katibu Mkuu MEAC Tanzania, Balozi wa
Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula.
Washiriki kwenye
mkutano huo kutoka Burudi walikuwa ni Waziri wa Biashara na Viwanda wa
Burundi Mhe.Mzigiyimana Marie Rose, Balozi wa Burundi nchini Marekani
Mhe. Ndabashinze Ernest, Ntibarutaye Glorioje ambaye ni mshauri ofisi ya
Wizara ya Biashara ya Burundi,
Wawakilishi kutoka
Kenya walikuwa ni James Kiiru amabaye ni Mkurugenzi masaidizi MFA &
IT Kenya, Balozi Nelson Ndirangu ambaye ni mkurugenzi MFA & IT
Kenya, Bi. Phylus Kandie Cabinet Secretary MEACT Kenya, Ronnie Gitonga
Naibu Katibu Ubalozi wa Kenya nchini Marekani na Esther Chemirmir PA to
CS MEACT Kenya.
Wawakilishi kutoka
Uganda walikua ni Balozi wa Uganda nchini Marekani Mhe. Alfred Nwam na
Stilson Muhwezi. Rwanda waliwakilishwa na Waziri wa Bisahara na Viwanda
Mhe. Robert Opirah na Innocent Kabandana.
Mkutano huo ni
mwendelezo wa ule mkutano wa mwishoni mwa mwaka jana nchi ya Marekani
ilipowaalika Marais wa Afrika katika mkutano kama huo ulioongozwa na
Rais Barack Obama.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269