Na Mwandishi Wetu
BENKI ya Posta Tanzania (TPB)
imedhamiria kuunganisha matawi yake yote katika mfumo wa kisasa wa
mawasiliano kupitia mkongo wa mawasiliano nchini (Fiber Optic) ili
kuberesha huduma na mawasiliano katika huduma zake.
Taarifa hiyo imetolewa jana jijini
Dar es Salaam na Meneja Mkuu Uendeshaji wa TPB, Kolimba Tawa alipokuwa
akizungumza katika makabidhiano ya mradi mpya wa benki hiyo
uliounganisha mawasiliano ya kisasa takribani matawi 11 maeneo
mbalimmbali nchini.
Tawa alisema mpaka sasa matawi ya
Arusha, Mbeya, Mwanza, Dodoma, Samora, Metropolitan, YWCA, Mkwepu,
Ubungo na Kijitonyama tayari yameunganishwa kwenye mfumo huo mpya na wa
kisasa kimawasiliano.
“..Mpaka hivi sasa matawi yetu
Kumi na Moja (11), yakiwemo Arusha, Mbeya, Mwanza, Dodoma, Samora,
Metropolitan, YWCA, Mkwepu, Ubungo, Kijitonyama, tayari zimeunganishwa
kwenye mfumo huo. Hii ni katika hatua ya mwanzo tu ya mradi huu, kwani
benki ya Posta imekusudia kuyaunganisa mtawi yake yote kwenye mfumo
huu,” alisema Tawa.
Alisema baada ya kukamilisha
matawi ya TPB katika mfumo wa Mkongo (Fiber Optic), imepata mafanikio
makubwa ukilinganisha na kipindi cha nyuma ambapo matawi haya yalikuwa
yameunganishwa na mtandao wa teknolojia ya Copper (Copper network).
Aidha akizitaja faida ambazo benki
hiyo imezipata baada ya kujiunga na Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano
unaosimamiwa na kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) ni pamoja kupungua kwa
msongamano wa wateja kusubiria huduma kwenye matawi, kuongezeka kwa
ufanisi na kupungua kwa dharura ya kusitisha huduma kwa muda.
“…Pia tumeboresha uwezekano wa
kutambua tatizo lolote linalotokana na kukatika kwa mawasiliano kwani
huu ni mfumo wa kidijitali…kupungua kwa gharama za uendeshaji katika
benki yetu.” alisema Tawa.
Kwa upande wao TTCL ikikabidhi
mradi huo kwa TPB, Mtatuzi wa Masuala ya Kiufundi, Fredrick Bernard
alisema mfumo huo wa mkongo unafaida kubwa kwani, mbali na kuwa salama
zaidi pia unauwezo wa kugundua tatizo la mawasiliano kabla ya kutokea
hivyo kufanyiwa kazi mapema.
Alisema hata hivyo alisema njia za
kupitisha mawasiliano hufanya kazi kwa kutegemeana na zipo zaidi ya
moja hali ambayo huwezesha hata njia moja kuisaidia nyingine inapopata
tatizo huku tatizo lililojitokeza likishughulikiwa kwa wakati huo.
Faida hizo pamoja na nyingine
nyingi zinaifanya benki ya Posta iamini kuwa huduma hii ya Mkongo
itolewayo na TTCL ni bora nchini na itatusaidia sana sisi benki ya Posta
kuboresha huduma zetu na kuongeza ufanisi katika shughuli zetu za
kibenki.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269