Breaking News

Your Ad Spot

Feb 18, 2015

Mzee Yusuph kuoa tena mke wa watatu,Wake zake watupiana vijembe mtandaoni

Mwimbaji mahiri wa muziki wa Taarab nchini ambaye pia ni mkurugenzi wa kundi la Jahazi Modern Taarabu,Mzee Yusuph anatarajia kuoa tena mke wa tatu hivi karibuni huku wake zake wawili wakiwa kwenye bifu zito wakitupiana vijembe mtandaoni.

Akipiga stori na Uheard na Soudy Brown alisema kuwa anatarajia kuoa mke huyo ambaye anaishi huko visiwani Pemba,na kwamba mipango ikiwa tayari kila kitu kitakuwa hadharani.

Hivi karibuni wake zake wawili ambao ni Malkia Leila Rashid ambaye pia ni mwimbaji wa kundi hilo na mke wake mdogo aitwaye Chiku wamekuwa wakirushiana vijembe kwenye mtandao wa kijamii wa ‘WathsAAp’ kwa kuandikiana ‘Status’ za vijembe.
           Mzee Yusuph akiwa na mke wake pili,Chiku.
Habari zinasema kuwa wake hao wamekuwa kama chui na paka na mzee Yusuph hana mpango wa kuwapatanisha kwa kuwa hakuna hata mmoja aliyeonyesha chuki kwa mwenzake akiwa na nao.
‘’Waache tu warushiane vijembe tena ndiyo vizuri na dawa yao nawaletea mke wa tatu na wala sina mpango wa kuwapatanisha,’alisema Mzee Yusuph

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages