BARAZA la Maadili ya Viongozi wa Umma, limemsomea rasmi mashitaka aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka (pichani), na kubainisha kuwa kiongozi huyo anastahili kujibu mashitaka kwa kosa la kuomba na kujipatia fedha kinyume na Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma.
Hata
hivyo, Profesa Tibaijuka alikana mashitaka hayo, na kusisitiza kuwa
hakukiuka maadili hayo ya viongozi wa umma, kwa kuwa fedha hizo
hakuziomba kwa maslahi yake binafsi, bali kwa ajili ya kuendeleza na
kuboresha taasisi yake inayotoa huduma ya elimu kwa watoto wa kike wasio
na uwezo lakini wenye vipaji.
Akimsomea
mashitaka hayo mbele ya baraza hilo, Mwanasheria wa Sekretarieti ya
Maadili ya Viongozi wa Umma, Wemaeli Mtei alisema Profesa Tibaijuka
ambaye ni kiongozi wa umma, alishawishi na kuomba fedha na baadaye
kupokea Sh bilioni 1.6 kutoka kwa James Rugemalira na mkewe.
Aidha,
Sekretarieti hiyo kupitia shahidi wake ambaye ni Katibu Msaidizi wa
Idara ya Viongozi wa Siasa kutoka Sekretarieti hiyo, Waziri Kipacha,
alisema kupitia Kamati ya Uchunguzi iliyoundwa na sekretarieti
kufuatilia sakata hilo, ilibaini kiongozi huyo aliomba na kupokea fedha
hizo kupitia barua aliyoandika Februari 4, mwaka 2012.
“Tulibaini
kuwa fedha alizoomba mlalamikiwa zilitumwa kwake kupitia akaunti yake
namba 00120102640201 ya Benki ya Mkombozi iliyopo St Joseph jijini Dar
es Salaam,” alisema huku akikabidhi baraza hilo barua hiyo ya Tibaijuka ya kuomba fedha na taarifa za kibenki kama ushahidi.
Alisema
pamoja na hayo, kamati hiyo pia katika uchunguzi wake ilibaini
mlalamikiwa ni mmoja wa wadhamini katika Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya
Barbro Johansson Girls Education Trust, ambapo barua kutoka Wakala wa
Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), ilithibitisha suala hilo. Na kwamba
wamiliki wa shule hiyo ndiyo wadhamini.
“Tumebaini
kuwa mlalamikiwa alipokea kiasi hicho cha fedha na wadhifa aliokuwa nao
kama Waziri, jambo lililomwingiza katika mgongano wa kimaslahi,” alisema.
Alisema
kitendo cha mlalamikiwa kupokea fedha hizo na kuingizwa katika akaunti
yake binafsi, ni kosa kwa mujibu wa masharti ya maadili ya viongozi wa
umma kwa kuwa viongozi wa umma hawaruhusiwi kuomba fedha au msaada au
kujipatia maslahi ya kiuchumi au kumpatia mtu mwingine maslahi hayo ya
kiuchumi.
Wakili
wa Tibaijuka, Dk Rugemeleza Nshara, alidai mbele ya Baraza mteja wake
hakuna kosa alilofanya, bali alitumia wadhifa alionao kama viongozi
wengine akiwemo Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kuomba na kuchangisha fedha
kwa ajili ya maendeleo ya wananchi na si binafsi.
“Nataka
kuuliza Baraza hili, ina maana juzi Waziri Mkuu, alivyoongoza
uchangishaji fedha kwa ajili ya maendeleo alikwenda kinyume na maadili
ya uongozi?,” alihoji.
Profesa Tibaijuka, alikiri kuomba fedha hizo kwa ajili ya kuendeleza taasisi hiyo yenye lengo la kujenga shule za mfano za wasichana wenyewe vipaji kila kanda ili kukuza na kuimarisha elimu ya mtoto wa kike nchini.
Profesa Tibaijuka, alikiri kuomba fedha hizo kwa ajili ya kuendeleza taasisi hiyo yenye lengo la kujenga shule za mfano za wasichana wenyewe vipaji kila kanda ili kukuza na kuimarisha elimu ya mtoto wa kike nchini.
“Huu
si msaada wa kwanza, tumekuwa tukifadhiliwa na Serikali ya Sweden
kupitia msaada tuliopatiwa na Rais mstaafu, Benjamin Mkapa, ambaye
alitambua juhudi zetu na kutuunga mkono, tumechangiwa na taasisi za
ndani na nje na watu binafsi, kiasi kinachohitajika kuboresha shule hizi
ni dola za Marekani milioni 14 sawa na takribani Shilingi bilioni
25.2,” alisema.
Alisema
pamoja na Rugemalira aliyetoa Sh bilioni 1.6, pia mfanyabiashara
maarufu nchini, Reginald Mengi alichangia taasisi hiyo Sh milioni 278,
ikiwemo Serikali ya Sweden iliyomaliza mkataba wake iliyochangia Sh
bilioni 8.1.
“Sisi
tuliopo kwenye taasisi hii, tunaaminiana na ni waadilifu ndiyo maana
fedha nilizoomba ziliingizwa kweli kwenye akaunti yangu lakini
niliziwasilisha, zilizobaki ni deni nililokuwa naidai taasisi, lakini
pia nimekopa Benki M Sh bilioni mbili kwa ajili ya kuboresha taasisi hii
na kuweka dhamana nyumba yangu iliyopo Oysterbay. Mbona hili
hamlioni?,” alihoji.
Wakati akijitetea, Tibaijuka aliomba akabidhi andiko lake mbele ya baraza hilo. “Nina
andiko langu na naomba nilikabidhi, kabla hujafa hujaumbika, nasimama
hapa leo kwa sababu tayari nimeshahukumiwa bila kusikilizwa, niliomba
hata bungeni nipewe nafasi lakini nilihukumiwa kama Waziri nikavuliwa
madaraka, nashangaa leo nimesimamishwa hapa kama mbunge,” alisema.
Alisema “mimi
mpaka sasa nasema sijakiuka maadili labda wanasheria wanieleweshe kwa
sababu nilisimama kama mimi wakati wa kuomba fedha na si kama waziri au
mbunge, hivyo sasa naona lengo ni kunivunja moyo, kunidhalilisha,
kunifanya kama mwanamke mhuni na tapeli.” Aliendelea kujitetea
"Nimekuja kujieleza ila.. Mimi siyo mwanasheria ila ukweli sina kosa na ndiyo maana nyaraka zote ambazo zipo hapa, mimi ndo nimewapa, nimekuja hapa kwa nia njema na naamini kwamba Baraza hili litanisikiliza kwa sababu ukweli ndiyo mwanzo wa maadili, lazima tupiganie haki na tupiganie ukweli.
"Nimekuja kujieleza ila.. Mimi siyo mwanasheria ila ukweli sina kosa na ndiyo maana nyaraka zote ambazo zipo hapa, mimi ndo nimewapa, nimekuja hapa kwa nia njema na naamini kwamba Baraza hili litanisikiliza kwa sababu ukweli ndiyo mwanzo wa maadili, lazima tupiganie haki na tupiganie ukweli.
“Kama
mimi nimefanya kosa kusimama kuwasaidia watoto wenye vipaji ni kosa,
naomba mwanasheria anieleweshe na naomba ukweli usimame maana tukienda
na fitina peke yake, hatutafika. Mimi ni profesa na mchumi na ni mstaafu
wa muda mrefu na nina pensheni, sina makuu, maisha yangu ni ‘simple’
(ya kawaida) huwezi kunikuta Dubai... Ila nipo tunafanya maendeleo na
wananchi wangu,” alisema.
Hata
hivyo alisema fedha anazodaiwa kuhamisha baada ya kupokea na kukatwa za
kulipa deni la Benki M, zilizobaki zilikuwa ni halali yake kwa kuwa
alikuwa akidai shule hivyo fedha hizo zilizobaki ni kwa ajili ya
matumizi yake binafsi.
“Mimi ni mchakarikaji, mtafuta fedha na kiongozi anayeshindwa kutafuta fedha kwa ajili ya watu wake hafai.
“Mimi ni mchakarikaji, mtafuta fedha na kiongozi anayeshindwa kutafuta fedha kwa ajili ya watu wake hafai.
"Hivyo
nilipolipwa milioni 117 (Shilingi), nilitoa milioni mbili nikachangia
Kanisa la Makongo na nikatoa laki nne nikapeleka kanisani na milioni 10
niliitoa kwa ajili ya matumizi yangu ya kununulia mboga, “ alisema.
Shahidi
wa Profesa Tibaijuka ambaye ni Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini wa Taasisi
hiyo, Balozi Paul Rupia katika ushahidi wake mbele ya Baraza, alisema
fedha hizo zimetafutwa na Profesa Tibaijuka.
Alisema
aliitaarifu bodi kwamba zipo fedha zimeingia katika akaunti yake na
zinatakiwa kulipa madeni wanayodaiwa. Alisema katika kikao hicho cha
kutoa uamuzi wa kugawanywa kwa fedha hizo kilichofanyika Luguruni ,
hakuhudhuria, ingawa alikuwa na taarifa zote za kinachoendelea.
Rupia
alisema bodi hiyo haikumpa masharti yoyote Profesa Tibaijuka ya
kumaliza kulipa madeni hayo kwa sababu hawakuona sababu ya kumfuatilia
kwa kuwa walimwamini, kutokana na juhudi zake binafsi za kupata fedha
hizo. Shauri hilo lilianza saa 3 na baadaye kuahirishwa kwa muda hadi
saa 6.30 mchana, lilipoanza kusikilizwa tena na kumalizika saa 11.45
jioni.
Katika
shauri hilo, Profesa Tibaijuka alitoa ushahidi kwa zaidi ya saa tatu,
akilalamika kuonewa na kuhukumiwa bila kusikilizwa. Shauri hilo
liliahirishwa hadi Machi 13 mwaka huu, kutokana na muda kutotosha.
Wakili aliomba udhuru wa kwenda Marekani kwa siku 10 na Jaji Msumi
alikubali.
Jaji Msumi alisema wajumbe watapitia shauri hilo na siku hiyo itaamuliwa, endapo hukumu itatolewa wazi au kwa uamuzi wa ndani.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269