RAIS MSTAAFU WA AWAMU YA PILI, ALI HASSAN MWINYI AZINDUA MAADHIMISHO YA WIKI YA SHERIA NCHINI
-Rais
Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi (wa pili kushoto)
akiongozana na jaji mkuu wa Tanzania, Mohamed Othaman Chande (watatu
kushoto) pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki (wa kwanza kushoto), Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu, na Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu,Shabani Ally LILA wakiwa
katika matembezi ya kuadhimisha wiki ya sheria nchini matembezi hayo
yalianzia katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kuishia katika
viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam February 1, 2015.
Bendi ya polisi ikiongoza matembezi ya wiki ya sheria nchini.
Watumishi
wa Mahakama nchini pamoja na watumishi wa taasisi zingine wakiwa wakiwa
katika matembezi ya kuadhimisha wiki ya sheria nchini matembezi hayo
yalianzia katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kuishia katika
viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam February 1, 2015.
Matembezi yakiwasili katika uwanja wa mnazi mmoja.
Vijana kutoka katika vikundi mbali mbali wakitoa burudani wakati wa kuadhimisha wiki ya sheria nchini.
Rais
Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi (wa kwanza kushoto),akipata
maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya
Afya (NHIF), Bw. Michael Mhando kuhusiana huduma wanazotoa NHF alipokuwa
akitembelea mabanda ya maonesho ya kuadhimisha wiki ya sheria nchini (kushoto katikati), jaji mkuu wa Tanzania, Mohamed Othaman Chande, na kulia Meneja Masoko na Elimu kwa Umma NHF, Bi. Anjela Mziray.
Wtumishi
wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),wakiendelea kutoa elimu kwa
washiriki wa maonesho hayo namna ya kujiunga na NHIF (wakwanza kulia), Afisa Masoko na Elimu kwa Umma wa NHIF, Bi. Catherine Kameka, na katikati Afisa Masoko na Elimu kwa Umma NHIF, Bi Hawa Duguza.
Washiriki wa maonesho hayo wakipata huduma mbalimbali kutoka kwenye banda la NHIF.
Rais
Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi akimsikiliza Naibu Msajili
wa Mahakama ya Rufaa, Bi. Zahra Maruma juu ya huduma zinazotolewa
alipotembelea banda hilo (wa kwanza kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam, Said Meck Sadiki.
jaji
mkuu wa Tanzania, Mohamed Othaman Chande akizungumza kabla ya
kumkaribisha mgeni rasmi Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan
Mwinyi kuzindua wiki ya sheria nchini yanayofanyika katika uwanja wa
mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.
Rais
Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi akitoa hotuba yake wakati
akizindua wiki ya sheria nchini katika uwanja wa mnazi mmoja jijini Dar
es Salaam.
Rais
Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi pamoja na Majaji waliokaa
mbele wakiwa kwenye picha ya pamoja na wakuu wa taasisi mbalimbali
zilizoshiriki katika wiki ya sheria nchini.
Rais
Mstaafu wa awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi ameitaka jamii kuacha
kuchukua sheria mkononi na badala yake waviache vyombo vya dola vifanye
kazi yao kwa mujibu wa sheria kwani kufanya hivyo ni jambo la dhuluma na
aibu.
Aliyasema hayo February 1, 2014 jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Mnazi Mmoja wakati akizindua maadhimisho ya wiki ya sheria nchini ambapo kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni "Fursa ya kupata haki: wajibu wa serikali,mahakama na wadau."
"ili Mahakama kutekeleza majukumu hayo lazima wananchi wajengewe uelewa juu ya shughuli za mahakama zinavyoendeshwa na hilo ndio lengo la maadhimisho haya,"Alisema Mwinyi Aliongeza kuwa ni vema wananchi wakajijengea utaratibu wa kuisadia mahakama pindi panapo hitajika ushahidi ili kuepuka kuachiliwa huru kwa wahalifu wao kwa kukosa ushahidi wa kutosha.
Alisema kuwa sheria pia inahitaji Majaji na Mahakimu watoe haki kwa kuzingatia sheria hivyo ni wajibu wa wananchi na jamii nzima kushirikiana na mahakama kupata haki halali kwa watuhumiwa wetu.Kwaupande wake Jaji Mkuu wa Tanzania Mohamed Chande Othman alisema kuwa mahakama imedhamiria kutoa elimu kwa ummma kuhusu masuala mbalimbali ya kimahakama.
Alisema kuwa wamejipanga katika kutoa elimu kuhusu ufunguaji na uendeshaji wa mashauri mbalimbali,utatuzi wa migogoro kwa njia ya suluhu muafaka pamoja na mfumo mpya wa kulipa tozo za mahakama kwa njia ya benki. "kwa mara ya kwanza mahakama ya tanzania imeamua kushirikisha jamii katika kujifunza jinjsi utendaji kazi wa mahakama unavyofanya kazi ni matumaini yetu kuwa jamii itajifunza vyema na kutii sheria za nchi"alisema Chande.













No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269