Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli
kushoto akimkaribisha Balozi wa Uingereza nchini Bi Dianna Melrose ofisini
kwake jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli (kulia) akizungumza na Balozi wa Uingereza nchini Bi. Dianna Melrose ofisini kwake
jijini Dar es Salaam kujadiliana mambo mbalimbali yahusuyo Miundombinu ya
Barabara za juu (flyovers), madaraja ya
chuma (mabey bridges) na suala zima la
kupunguza msongamano katika jiji la Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi Dkt.
John Pombe Magufuli (kulia) akisalimiana na Richard Boulter kutoka Idara ya
Maendeleo ya Kimatifa ya Uingereza (Department
for International Development) aliyeambatana na Balozi wa Uingereza nchini
Bi. Dianna Melrose.
Majadiliano
yakiendelea kati ya Ujumbe wa Balozi wa Uingereza nchini, Bi Dianna Melrose pamoja na Waziri wa Ujenzi
Dkt. John Pombe Magufuli.
Ujumbe kutoka Ubalozi
wa Uingereza nchini, wakwanza kulia ni Balozi wa Uingereza Dianna Melrose, anayefuatia
ni Meneja wa Masula ya Biashara na Maendeleo Marie Strain pamoja na Richard
Boulter kutoka Idara ya Maendeleo ya Kimatifa ya Uingereza. (Picha zote kwa
Hisani ya Kitengo cha Mawasiliano Serikalini (GCU)-Wizara ya Ujenzi)
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269