Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger
amekiri kuwa amekuwa akichezesha kikosi hafifu katika michuano ya FA
ilikuimarisha ushindani wa the Gunners katika kombe la mabingwa Ulaya
Habari inawadia wakati the Gunners
wanajiandaa kukabiliana na Manchester United, kuwania taji la FA katika
hatua ileile walioambulia kichapo cha 4-0 katika msimu wa mwaka wa 2008.
Mechi hiyo ilikuwa imekaribiana sana na mechi yao ya mchujo wa kombe la kuwania ubingwa wa barani ulaya dhidi ya AC Milan.
"Ni wazi iwapo ratiba ya mechi ya FA
imewekwa karibu sana na mechi za kuwania ubingwa wa bara ulaya kama
kocha ni wajibu wao kubaini ipi kati ya mechi hizo ni muhimu.'' alisema
Wenger.
''kama unawachezaji wazuri unawapumzisha na badala yake kuwachezesha wengine katika mchuano wa FA.
Wenger alifanya mabadiliko katika
kinyang'anyiro cha mwaka wa 2008 akiwapumzisha wachezaji wanne wa
kutegemewa na licha ya kichapo hicho dhidi ya United walifaulu kufuzu
kwa robo fainali ya kombe la mabingwa barani Ulaya baada ya kutoka sare
tasa na timu hiyo ya Italia.
Tofauti na mwaka huo msimu huu vijana wa
Wenger wanamlima wa kukwea baada ya kuambulia kichapo cha 3-1 mikononi
mwa Monaco katika mkondo wa kwanza wa raundi ya kumi na sita bora
uwanjani Emirati.
Hawatakuwa na mechi nyengine hadi tarehe
17 mwezi huu na hivyo huenda ikamruhusu Wenger ama Professa Wenger
kuwachezesha nyota wake wa kutegemewa bila ya hofu ya kuwapoteza kwa
majeraha.
Iwapo hali ni shwari Wenger huenda akawania ushindi wake wa kwanza uwanjani old Trafford tangu mwaka wa 2006.
Wenger anaamini kuwa matokeo ya mechi
hiyo ya FA itaisaidia Arsenal kubaini kasi yake katika uwaniaji wa
nafasi nne bora katika ligi kuu ya Premia.
Arsenal inaalama moja pekee mbele ya United ambayo inashikilia nafasi ya nne katika jedwali la ligi kuu ya Premia ya Uingereza.
Wenger "mechi ya jumatatu itakuwa mechi
ya kukata na shoka maanake iwapo timu inashinda mechi kubwa na yenye
hadhi kama hii wachezaji wake huwa wanaimarika kisaikolojia na motisha
wao unawasaidia kushinda mechi zaidi''
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269