Mwigizaji wa vichekesho wa Kundi la Orijino Komedi, Mujuni
Sylivery aka Mpoki moja ya vitu ambavyo aliwahi kuvifanya katika kazi
yake ya uchekeshaji ni pamoja na kuigiza sauti ya marehemu, Kapteni John
KOMBA ambaye amefariki February 28.
Leo Mpoki amesikika kwenye Leo Tena CloudsFM, alianza kuzungumzia namna alivyopokea taarifa za msiba huo; “..Mtu
akishatoweka kwenye ulimwengu akifariki dunia inauma kwa sababu mtu
unayempoteza leo huwezi kumpata tena.. lakini ukimpoteza mbuzi utaenda
Vingunguti utamnunua na sherehe itaendelea.. Kitendo cha kufariki mtu
yoyote hata kama hajulikani ni pengo kubwa tu”
“Imeniathiri
kwa kisanii kwa kuwa nilikuwa namuwezea, kidogo alikuwa hapendi lakini
ilivyokuja akatulia.. Watu wakamwambia bwana hawa watoto tu.. Ukimuiga
mtu ana mazuri huwezi kumuiga kwa mabaya tu.. ana mazuri yake..Ikanipa
wigo mpana kwenye kazi yangu ya kubuni sauti yake, vitendo..“
“mwisho
wa siku kaondoka pengo lake halitozibika.. Kama kuna la kufanya kuhusu
yeye kwa kumuenzi sitokuwa nyuma, nitafanya ili mradi lisimvunjie
heshima Marehemu, familia yake, jamii, viongozi wenzake Bungeni na watu
wote ambao kawaacha kwenye jimbo lake sasa hivi wapweke..“
Mpoki
alikuwa akimuigiza marehemu Komba, na Komba hakuwa natatizo nae ila
alimshauri awe anavaa na kuonekana mtannashati wakati anamuigiza kwani
yeye (marehemu ) alikuwa ni mtanashati, Komba aliyasema hayo mwaka jana
kwenye kipindi cha Mkasi.
Picha:Mpoki akiwa na baadhi ya waigizaji wenzake leo katika viwanja vya karimjee walipokuwa wakiuaga mwili wa Komba.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269