Breaking News

Your Ad Spot

Mar 17, 2015

MTOTO AZALIWA BILA UBONGO WA NYUMA

Na Haruni Sachawa
NImaajabu! Mwanamke mmoja, Diana Dioniz  mkazi wa Magomeni Makuti jijini Dar es Salaam, ameangua kilio cha kuomba msaada baada ya mtoto wake aliyezaliwa mwaka mmoja uliopita kugundulika kuwa hana ubongo wa nyuma (medulla oblongata), hali inayosababisha shingo kulegea na macho kutoona.

Mtoto anayedaiwa kuzaliwa bila ya ubongo wa nyuma(medulla oblongata).
Akizungumza na gazeti hili nyumbani kwake, Diana alisema alipata ujauzito wa mtoto huyo na kujikuta akiwa na furaha kubwa, lakini baada ya kuzaliwa na kumpa jina la John, amejikuta akipata mateso makubwa, kwani kwa muda wote, shingo yake inakuwa imelegea na macho yake hayaoni.
“Majirani walinishauri nimpeleke hospitali kwa uangalizi zaidi, nilipomfikisha Muhimbili nikaambiwa suala la mwanangu linapaswa kushughulikiwa na daktari bingwa wa magonjwa ya watoto wa Kitengo cha Moi,” alisema mwanamke huyo.
Aliongeza kuwa, baada ya kupelekwa huko na kuchunguzwa ndipo ilipojulikana kuwa na matatizo hayo, ambayo yamemfanya kuwa na wakati mgumu katika kumlea, kwani analazimika kuwa naye karibu kwa muda wote, jambo linalomfanya kukosa muda wa kufanya majukumu mengine.
Mtoto huyo akiwa na mamayake.
“Hali yangu ya kimaisha ni ngumu sana, sina msaada wowote hapa, nakaa kwa bibi mzaa baba, mama yangu yuko kwao, kwa sababu walishaachana na baba yangu  muda mrefu na kwa sasa  baba ana familia kubwa huko Mwanza.
“Ninawaomba Watanzania wanisaidie ili mtoto aweze kukaa, pia naomba pesa kwa ajili ya kumhudumia kupata  maziwa na matumizi mengine kama kiti cha magurudumu (wheelchair). Aliyeguswa na habari hii awasiliane nami kwa simu namba 0718 690219,” alisema Diana.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages