Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed
Shein (katikati) akijumuikana Viongozi na waislamu katika kisomo cha
Hitima ya Marehemu Salmin Awadh aliyekuwa Mwakilishiwa Jimbo la Magomeni
(CCM) iliyosomwa leo jioni katika Msikiti wa Mushawal, Mwembeshauri
Mjini Unguja. Hitma hiyo ilihudhuriwa na Waumini na Wanachama wa Chama
cha Mapinduzi. (PICHA ZOTE NA IKULUR)
Baadhi
ya Waislamu, viongozi mbalimbali na wananchi, wakiwa katika kisomo cha
Hitima ya kumuombea Marehemu Salmin Awadh aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo
la Magomeni (CCM), Mjini Unguja aliyefariki hivi karibuni. Hitima hiyo
ilisomwa leo jioni katika Msikiti wa Mushawal Mwembeshauri.
Katibu
wa Mufti Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Fadhil Soraga akitoa mawaidha baada
ya kisomo cha Hitima ya Marehemu Salmin Awadh, aliyekuwa Mwakilishi wa
Jimbo la Magomeni (CCM), Mjini Unguja aliyefariki hivi karibuni. Hitima
hiyo ilisomwa leo jioni katika Msikiti wa Mushawal Mwembeshauri
Naibu
Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai akitoa shukurani kwa Viongozi
mbalimbali, Waislamu na Wananchi na wapenzi wa CCM baada ya kisomo cha
Hitima Marehemu Salmin Awadh aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni
(CCM) Mjini Unguja iliyosomwa leo katika Msikiti wa Mushawal
Mwembesahauri. Marehemu alifariki hivi karibuni na kuzikwa Makunduchi,
Mkoa wa Kusini Unguja.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269