Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata
maelezo toka kwa Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe Benson Mpesya juu ya
madhara makubwa ya mali na maisha ya watu wakati wa ziara maalum ya
kutoa pole kwa wahanga wa mvua iliyoandamana na mawe na kusababisha
upotevu wa maisha ya watu na uharibifu mkubwa wa mali katika vijiji
vitatu vya Kata ya Mwakata, Wilaya ya Kahama, Mkoa wa Shinyanga.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akizungumza na familia zilizoathirika na mvua kali iliyoandamana na
mawe na kusababisha upotevu wa maisha ya watu na uharibifu mkubwa wa
mali katika vijiji vitatu vya Kata ya Mwakata, Wilaya ya Kahama, Mkoa wa
Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akikagua baadhi ya makazi ya dharura kwa familia zilizoathirika na mvua
kali iliyoandamana na mawe na kusababisha upotevu wa maisha ya watu na
uharibifu mkubwa wa mali katika vijiji vitatu vya Kata ya Mwakata,
Wilaya ya Kahama, Mkoa wa Shinyanga.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa
pole kwa familia zilizoathirika na mvua kali iliyoandamana na mawe na
kusababisha upotevu wa maisha ya watu na uharibifu mkubwa wa mali katika
vijiji vitatu vya Kata ya Mwakata, Wilaya ya Kahama, Mkoa wa Shinyanga.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwapa
mkono wa pole waalimu wa shule ya msingi ya Mwakata, wilaya ya Kahama,
Mkoa wa Shinyanga, ambao pia ni waathirika wa mvua kali iliyoandamana
na mawe na kusababisha upotevu wa maisha ya watu na uharibifu mkubwa wa
mali katika vijiji vitatu vya Kata ya Mwakata, Wilaya ya Kahama, Mkoa wa
Shinyanga.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akihutubia mamia ya wananchi baada ya kutembelea na kuzifariji familia
zilizoathirika na mvua kali iliyoandamana na mawe na kusababisha upotevu
wa maisha ya watu na uharibifu mkubwa wa mali katika vijiji vitatu vya
Kata ya Mwakata, Wilaya ya Kahama, Mkoa wa Shinyanga.
……………………………………………………………………………….
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Alhamisi, Machi 12,
2015, amefanya ziara maalum ya kutoa pole kwa wahanga wa mvua
iliyoandamana na mawe na kusababisha upotevu wa maisha ya watu na
uharibifu mkubwa wa mali katika vijiji vitatu vya Kata ya Mwakata,
Wilaya ya Kahama, Mkoa wa Shinyanga.
Rais Kikwete amewasili mjini Kahama kiasi cha saa nane mchana
baada ya ndege yake kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Mgodi wa Buzwagi na
kwa muda wa kiasi cha saa tatu ametembelea familia ambazo zimepata
madhara makubwa zaidi kutokana na mvua hiyo iliyonyesha kwa kiasi cha
saa moja tu kuanzia saa nne usiku Machi 3, mwaka huu, 2015 na kuambana
na upepo mkali na mawe.
Watu 47 walipoteza maisha, 112 wakaumia, nyumba 657 zikabomolewa
ama kuharibiwa na kaya 468 kuathirika katika vijiji vitatu vya Kata ya
Mwakata na tokea siku ya maafa, Serikali imetoa huduma za dharura za
chakula, sehemu za kulala, huduma za afya na huduma nyingine muhimu kwa
binadamu.
Baada ya kupatiwa maelezo ya kina na uongozi wa Mkoa wa
Shinyanga chini ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mheshimiwa Ali N. Lufunga,
Rais Kikwete ameanzia ziara yake katika Kijiji cha Maghuhumwa, nyumbani
kwa Bwana Masemba Maburi, ambaye alipoteza watoto watano katika maafa
hayo. Rais Kikwete ametoa pole kwa wafiwa na kuzungumza na wananchi
waliokuwepo kwenye msiba.
Bwana Maburi ambaye sasa anaishi katika nyumba ya jirani pamoja
na familia yake na familia nyingine tatu amemweleza Rais Kikwete jinsi
nyumba mbili ambako watoto hao na mama yao walipokuwa wamelala
zilivyoanguka na mama huyo akalazimika kukimbilia nje kwa nia ya
kutafuta msaada lakini watoto wakazidiwa na kupoteza maisha.
“Sijawahi kuona mvua kubwa, kali na yenye upepo mkali kiasi kile
katika maisha yangu. Mvua ilianza saa nne usiku na ikanyesha kwa muda
mfupi sana, nyumba zikaanguka ama kubomolewa. Jameni tusaidie kwa sababu
tumekwazika,”Bwana Maburi amemwambia Rais Kikwete.
Baada ya kutoka katika Kijiji cha Maghuhumwa, Rais Kikwete
amekwenda katika Kijiji cha Nhumbi ambako amempa pole Bwana Zacharia
Limbe na familia yake ambayo ilipoteza wajukuu wanne katika maafa hayo
ya mwanzoni mwa mwezi huu.
Akiwa nyumbani kwa Bwana Limbe, Rais Kikwete ametembea na
kujionea makazi mapya ya dharura ya familia ambayo yamejengwa kwa msaada
wa Serikali.
Baada ya kuondoka kwa Bwana Limbe, Rais Kikwete ametembelea eneo
la makazi ya walimu wa Shule ya Msingi ya Mwakata, ambako walimu hao
wamehifadhiwa katika fremu za maduka kutokana na athari za maafa hayo.
Rais Kikwete amewapa pole walimu hao na kuwaambia: “Pole sana. Tuko
pamoja. Tutaendelea kusaidiana kuona jinsi gani mnavyoweza kurejea
katika maeneo yenu ya makazi ya kawaida.”
Rais Kikwete ataondoka kesho, Ijumaa, Machi 13, 2015, kurejea
Dar es Salaam baada ya ziara hiyo maalum ya siku mbili katika Mkoa wa
Shinyanga.
………………………..
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
12 Machi, 2015
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269