Watu
42 wamepoteza maisha na wengine 82 kujeruhiwa baada ya mvua ya upepo
mkali kusababisha mafuriko katika kata ya mwakata wilayani Kahama mkoani
Shinyanga.
Mvua
hiyo ambayo ilinyesha kwa muda mfupi imewaacha watu 3,500 bila makazi
katika kaya 350 huku nyumba zikifurika maji na baadhi ya mifugo
ikisombwa.
Mkuu
wa mkoa wa Shinyanga Bw. Ali Nasoro Rufunga amesema mvua hiyo ya mawe
iliyoambatana na upepo mkali ilisababisha mafuruko katika kata ya
Mwakata kuezua nyumba na nyingine kuanguka.
Amesema
mali mbalimbali zimeharibiwa vibaya ikiwemo mifugo kuzolewa na maji na
vyakula kwenye eneo lote lililokumbwa na mafuriko hayo.
Hali ya majeruhi ambao wamepelekwa katika hospitali mbalimbali bado sio nzuri kwa baadhi ingawa wengine wanaendelea vizuri.
Miili ya watu 7 wa familia moja waliokufa katika tukio hilo
Raha ya milele uwape bwana..
ReplyDelete