KLABU
ya Simba ya jijini imewasili visiwani Zanzibar tayari kwa maandalizu ya
mchezo wake na Yanga unaotarajiwa kufanyika jumapili ijayo katika
Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salam.
Kikosi
cha watu 28, wakiwemo viongozi, madaktari na wajumbe wa dawati la
ufundi kimeiwasili visiwani Zanzibar, majira ya saa 8.35 mchana bila ya
Kocha Mkuu timu hiyo, msaidizi wake Suleiman Matola na Simon Sserenkuma,
ambao wataungana na kikosi hicho mara baada ya kumalizika kwa matatizo
binafsi wanayokabiliana nayo.
Akizungumza
na mwandishi wa habari hizi, Mjumbe wa Kamati Tendaji ya klabu hiyo,
aliyepo Zanzibar Abdul Mshangama, amesema kuwa Matola amebakia jijini
Dar es Salama kutokana na kukabiliwa na matatizo ya kifamilia sawa na
Sserenkuma aliyepo nchini kwao, Uganda na kwamba wawili hao
wangelijiunga pamoja na kocha mkuu wa timu, Goran kopunovic ambao
wangewasili usiku wa leo au kesho asubuhi.
Mshangama
alisema mbali ya kuwa ni kawaida ya klabu hiyo kupiga kambi visiwani
humo kila inapokuwa na mechi kubwa kama ya Jumapili, kambi hiyo ya siku
7, itakuwa maalum kutokana na ukubwa wa mechi inayowakabili.
Alisema
ingawa mchezo huo ni wa kawaida kama ilivyo michezo mingine ya Ligi Kuu
ya Tanzania Bara, mchezo huo unapewa umuhimu mkubwa baada ya timu hiyo
kuibuka na ushindi wa magoli 5 – 0 dhidi ya Prison ya Mbeya.
“Tunashukuru
timu imewasili salama na kufika katika kambi yetu ya kawaida na
wachezaji wote isipokuwa SIMON (Sserenkuma) ambaye atawasili Dar es
salam kesho jioni na ataungana na wenzake usiku au keshokutwa asubuhi”,
alisema Mshangama.
Mjumbe
huyo alisema mazoezi ya timu hiyo yanayotarajiwa kufanyika katika
Kiwanja cha Chuo cha Kiislamu Chukwani na Uwanja wa Amaan yataendelea
hadi Jumamosi na katika kipindi hicho, timu hiyo inatarajia kucheza
mechi mbili za majaribio kabla ya timu hiyo haijarudi jijini Dar es
Salam siku inayofuata moja kwa moja hadi uwanjani kwa ajili ya mchezo
huo.
“Mipango
ya timu ni kubakia hapa hadi siku moja kabla ya mchezo au siku ya
mchezo na baadaye kurudi jijini na kufikia Uwanjani”, aliongeza
mshangama aliyekuwa ameambatana na baadhi ya wadau wa timu hiyo huku
wachezaji na walimu wakianza safari ilipo kambi ya timu hiyo.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269