Breaking News

Your Ad Spot

Mar 3, 2015

YATIMA KUJENGEWA NA GOLA FOUNDATION

 Kikundi cha ngoma cha watoto wa mitaani wakitumbuiza katika shughuli ya kuwakusanya watoto wa mitaani iliyofanywa na taasisi ya GOLA Foundation inayolenga kuwasaidia watoto wa mitaani kukabiliana na changamoto za ukosefu wa malazi,chakula,mavazi na pia elimu.Jamii inaombwa kujitokeza kusaidia watoto hao
Baadhi ya Watoto wa mitaani waishio jijini Arusha waliokusanywa na  taasisi ya GOLA Foundation inayolenga kuwasaidia watoto wa mitaani kukabiliana na changamoto za ukosefu wa malazi,chakula,mavazi na pia elimu.Jamii inaombwa kujitokeza kusaidia watoto hao


Watoto wa mitaani wanaoishi  jijini Arusha katika mazingira hatarishi wanatarajiwa kujengewa Hostel zitakazowasaidia kuondokana na adha ya kupata sehemu za malazi hivyo kulazimika kulala maeneo ya stendi za mabasi na masoko.

Mkurugenzi wa shirika la Gola linalojihusisha na masuala ya watoto wa mitaani jijini Arusha,Sawale Maghema  amesema kuwa mpango huo utasaidia watoto wa mitaani kuondokana na mazingira magumu yanayowapelekea kujiingiza katika vitendo vya uhalifu na matumizi ya madawa ya kulevya.

Sawale alisema kuwa iwapo watoto wa mitaani watatelekezwa na jamii bila kusaidiwa wanaweza kugeuka na kuwa mwiba kwa jamii ya Watanzania hivyo amewataka Watanzania kujitokeza kuwasaidia watoto hao .

"Watoto wa mitaani tuna mpango maalumu wa kuwakusanya na kuwakutanisha pamoja kujua mahitaji yao ,malengo na matarajio waliyonayo ili kuwasaidia kwa kushirikiana na jamii hata kwa hili la ujenzi wa Hostel litasaidia kuwaweka pamoja tukiwaacha waendelee kukaa mitaani hawatabadilika wataendelea kuwa na maisha mabaya" Alisema Sawale

Mdau wa Masuala ya utalii Mustafa  Panju  alijitolea kuwasaidia watoto wa mitaani kwa kuchangia kiasi cha shilingi milioni 20 kwa watoto hao ili waweze kupata mahitaji muhimu  ,Ameeleza kuwa jamii inapaswa kuamka na kuwasaidia watoto hao badala ya kuwaacha waendelee kukaa kwenye mazingira hatarishi.

Mwenyekiti wa Baraza la Watoto Arusha ,Hassan Omari akizungumza kwa niaba ya watoto wa mitaani anaeleza kuwa watoto wa mitaani wana ndoto nyingi,vipaji na uwezo wa hali ya juu hivyo wakisaidia wanaweza kufika mbali na kulisaidia taifa .

Chanzo:libeneke la kaskazini blog

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages