Breaking News

Your Ad Spot

Mar 27, 2015

ZIARA YA KATIBU MKUU WA CCM NDUGU KINANA NDANI YA JIMBO LA SAME MAGHARIBI MKOANI KILIMANJARO

 
 ,Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana ukielekea katika kijiji cha Gonjanza kata ya Suji,kuzindua mradi wa masi safi na salama sambamba na kuzungumza na wananchi,wilaya ya Same Magharibi mkoani Kilimanjaro.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimpungia mkono mkazi wa kijiji cha Gonjanza kata ya Suji,Msafara wa Kinana ulikuwa ukielekea katika hicho kuzindua mradi wa masi safi na salama sambamba na kuzungumza na wananchi,wilaya ya Same Magharibi mkoani Kilimanjaro. 
Katibu Mkuu yupo kwenye ziara ya kuimarisha Chama cha Mapinduzi ikiwa pamoja na kukagua,kusimamia na kuhimiza ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010.
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Mbunge wa Jimbo la Same Magharibi Dk.David Mathayo David wakinywa maji ya bomba mara baada ya Katibu Mkuu kuzindua mradi wa maji safi na salama kwa wananchi wa kijiji cha Gonjanza kata ya Suji
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akimtiwsha ndoo ya maji mkazi wa kijiji cha Gonjanza kata ya Suji
 wakazi wa kijiji cha Gonjanza kata ya Suji wakifurahia kupatikana kwa maji katika kijiji hicho,ambapo Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Mbunge wa Jimbo la Same Magharibi Dk.David Mathayo David walizindua mradi huo 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akijibu baadhi ya changamoto za wananchi wa Hedaru waliomsomea kwenye risala yao, Katibu Mkuu alipita Hedaru kushiriki na kukagua ujenzi wa ofisi ya CCM kata ya Hedaru.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Same Magharibi Dk. David Mathayo David wakati wa mapokezi katika kata ya Njoro .Katibu Mkuu yupo kwenye ziara ya kuimarisha Chama cha Mapinduzi ikiwa pamoja na kukagua,kusimamia na kuhimiza ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010.

 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wananchi wa kata ya Njoro ikiwa ni kituo cha kwanza katika ziara ya Katibu Mkuu wa CCM jimbo la Same Magharibi. 
  Wananchi wa kata ya Njoro wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipokuwa akiwapongeza kwa uamuzi wao wa kujenga shule ya sekondari katika kata yao.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kupanda miti kwenye eneo la shule ya sekondari ya Njoro,jimbo la Same Magharibi ikiwa sehemu ya utunzaji mazingira.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Mbunge wa Jimbo la Same Magharibi wakishiriki ujenzi wa madarasa ya shule ya sekondari ya kata ya Njoro. 
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wajumbe wa mkutano mkuu wa jimbo la Same Magharibi na kuwataka wajumbe hao kuhimiza umoja kati ya wana CCM na kuwapongeza kwa ushindi mzuri wa serikali za mitaa. Katibu Mkuu pia alisisitiza kuwa kutokana na tatizo la maji kuwa kubwa nchi,CCM itahakikisha kwenye ilani yake mpya kuipa kipaumbele cha kwanza maji safi na salama kwa watanzania.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akipiga gitaa wakati wa mkutano wa kuwasalimia wananchi kijiji cha Makanye ,jimbo la Same Magharibi.  

 wanancho wakifurahia jambo 
   Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Katibu wa NEC Itikadi na Unezi Nape Nnauye wakiwa wameongozana na wananchi katika kijiji cha Gonjanza kata ya Suji,wakielekea kuzindua mradi wa maji
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kufukia mabomba ya maji katika kijiji cha Gonjanza pamoja na Mbunge wa Jimbo la Same Magharibi Dk.David Mathayo David

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages