Breaking News

Your Ad Spot

Apr 24, 2015

ASKARI POLISI KUUWAWA NA WANANCHI HUKO MOROGORO

Askari mmoja wa jeshi la polisi ambao hutumia pikipiki kufanya doria, aliyejulikana kwa jina la Ramadhani, ameuawa mchana huu na wananchi wenye hasira mjini Morogoro kwa kutuhumiwa kusababisha ajali ya dereva wa bodaboda ambaye aliparamia lori.
Tukio hilo linawahusisha askari wawili wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) waliokuwa wakiendesha pikipiki yenye namba za usajili za PT 823 ambayo ni mali ya polisi.
Mashuhuda wamesema kwamba polisi hao walikuwa wakimfukuza dereva huyo wa bodaboda ambaye alikwenda kujikita katika lori ambapo wananchi waliwatuhumu kusababisha ajali hiyo na kuanza kuwashambulia.
Baada ya kuona hivyo, polisi hao walianza kurusha risasi hewani lakini wananchi waliwakabili kwa kuwarushia mawe na hivyo kumwua polisi mmoja

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages