Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe ambaye alikuwa mgeni rasmi
akiongea katika Tamasha la kumi na tano la Pasaka ililofanyika katika
Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, Jumapili 5, 2015. Pembeni ni
Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama.
…….
PICHA ZOTE NA CATHBERT KAJUNA WA KAJUNASON BLOG.
Mkurugenzi wa Msama Promotion,
Alex Msama akiwapungia watu waliohudhuria katika Tamasha la kumi na tano
la Pasaka, lililofanyika katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam,
Jumapili 5, 2015.
Askofu David Mwasota wa Kanisa
la Naioth Gospel Assembly akisoma hotuba amempongeza Mhe. Bernard Membe
kwa kujumuika na Watanzania katika Tamasha la kumi na tano la Pasaka
ililofanyika katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, Jumapili 5,
2015.
Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe akiwa na Waziri wa
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Fenella Mukangara (kulia),
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Angella
Kairuki na Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama na Mkewe.
Watu waliohudhuria Tamasha la
kumi na tano la Pasaka, lililofanyika katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar
es Salaam, Jumapili 5, 2015.
Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe akitoa vyeti vya
shukrani kwa vyombo mbali mbali vya habari vilivyoshiriki kwa miaka
kumi na tano katika kulitangaza tamasha la Pasaka.
Tuzo ya heshima ilitolewa kwa Rais Mstaafu, Mhe. Ali Hassan Mwinyi.
Mhe Bernard Membe alitunukiwa tuzo kwa mchango wake kwa shughuli za kijamii.
Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe akishirikiana na
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Fenella Mukangara
(kulia) na Mchungaji Mwasota kukata keki. Aanayeshudia ni Naibu Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Angella Kairuki.
Mgeni
rasmi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard
Membe akimlisha keki Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama na mkewe.
Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe akimlisha keki Naibu
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Angella Kairuki.
Pembeni anayeshuhudia ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo,
Mhe. Fenella Mukangara.
Mwimbaji wa muziki wa injili
kutoka nchini Afrika Kusini anayefahamika kwa jina la Rebbeca Malope
akitoa burudani katika Tamasha la kumi na tano la Pasaka, lililofanyika
katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, Jumapili 5, 2015.
Mwimbaji wa muziki wa injili kutoka nchini Afrika Kusini, Mchungaji Solly Mahlangu mwanamuziki nguli akiimba na kucheza katika Tamasha la kumi na tano la Pasaka, lililofanyika katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, Jumapili 5, 2015.
Mwimaji Chritina Shusho akiimba
katika Tamasha la kumi na tano la Pasaka, lililofanyika katika Uwanja wa
Taifa, jijini Dar es Salaam, Jumapili 5, 2015..
Mwimbaji Rose Mhando akiwasha
moto wa kamata pindo la Yesu katika Tamasha la kumi na tano la Pasaka,
lililofanyika katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, Jumapili 5,
2015.
Wakiimba kwa pamoja…
Msanii wa Sarakasi akitoa
burudani katika Tamasha la kumi na tano la Pasaka, lililofanyika katika
Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, Jumapili 5, 2015.
Mwimbaji John Lissu na waimbaji wake wakiimba.
Mwimbaji wa Nyimbo za Injili, Joshua na vijana wake wakiimba.
Kwaya ya Kijitonyama wakiimba
katika Tamasha la kumi na tano la Pasaka, lililofanyika katika Uwanja wa
Taifa, jijini Dar es Salaam, Jumapili 5, 2015.
Kwaya ya Kijitonyama Upendo
Group ikiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuimba katika Tamasha
la kumi na tano la Pasaka, lililofanyika katika Uwanja wa Taifa, jijini
Dar es Salaam, Jumapili 5, 2015.
Marafiki wakifurahia…
Mtangazaji wa Clouds Radio & TV, Samweli Sasali akiongea na waimbaji wa Kwaya ya Kijitonyama Upendo Group…
Taswira ikitafutwa…
……………………………………………………………………………………….
Na Mwandishi Wetu, Dar.
Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe ametoa rai kwa viongozi wa
dini zote pamoja serikali kuhimiza vijana waipende dini ili kudumisha
amani, utulivu na uadilifu.
Mhe Membe amesema hayo wakati
akihubutibi maelefu wa watu waliohudhuria Tamasha la kumi na tano la
Pasaka, lililofanyika katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam,
Jumapili 5, 2015.
Askofu David Mwasota wa Kanisa
la Naioth Gospel Assembly akisoma hotuba amempongeza Mhe Bernard Membe
kwa kujumuika na Watanzania katika Tamasha la kumi na tano la Pasaka.
Katika Tamasha hilo la Pasaka,
Kampuni ya Msama Promotions, ambao ndio waandaji wa Tamasha hilo,
wamemtunuku Mhe. Rais Jakaya Kikwete kwa mchango wake katika kukuza
tasnia ya Sanaa nchini.
Tuzo ya heshima ilitolewa kwa Rais Mstaafu, Mhe. Ali Hassan Mwinyi.
Mhe Bernard Membe alitunukiwa tuzo kwa mchango wake kwa shughuli za kijamii.
Tuzo zimetolewa kwa vyombo mbalimbali vya habari nchini kwa michango yao katika kutangaza Tamasha la Pasaka.
Viongozi wa Serikali
waliohudhuria Tamasha hilo ni pamoja na Mhe. Fenella Mukangara, Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Angela Kairuki, Naibu
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, naMhe. Paul Makonda,
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni.
Tamasha hilo lilihudhuriwa na
viongozi wa kidini wakiwemo, Askofu David Mwasota wa Kanisa la Naioth
Gospel Assembly na Mchungaji Mwasota.
Tamasha la Pasaka lilianzishwa
rasmi mwaka 2000 na huwashirikisha Waimbaji wa Nyimbo za Injili kutoka
nchini na nje ya nchi ambapo mwaka huu limewashirikisha waimbaji kutoka
hapa nchini, Afrika Kusini, Uingereza na Zambia.
Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe akiwa na Naibu
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Angella Kairuki na
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda wakifuatilia tamasha.
Mshehereshaji akiendesha Tamasha
la kumi na tano la Pasaka, lililofanyika katika Uwanja wa Taifa, jijini
Dar es Salaam, Jumapili 5, 2015.
Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe akiondoka pamoja na
wageni wake mara baada ya kuhutubia.
Nikiripoti toka Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ni Mimi Cathbert Angelo Kajuna wa Kajunason Blog…
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269