Breaking News

Your Ad Spot

Apr 2, 2015

COASTAL YAIPIGIA HESABU PRISON, YAWEKA MIPANGO YA KUHAKIKISHA POINTI TATU ZINABAKI MKWAKWANI.


unnamed
wachezaji wa Coastal Union wakiwa na mazoezi jana kwenye viwanja vya shule ya sekondari Popatlaly chini ya Kocha Mkuu Jamhuri Kihwelu “Julio”,
………………………………………………….
NA MWANDISHI WETU, TANGA
Timu ya Coastal Union ameanza kuzipigia hesabu pointi tatu muhimu za wapinzani wao Tanzania Prison ili kuweza kuhakikisha wanazichukua wakati watakapokutana kwenye mechi ya Ligi kuu Tanzania bara.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa wikiendi hii kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani ikiwa ni mzunguko wa pili wa ligi hiyo ikielekea lala salama.Akizungumza leo mara baada ya kumalizika kwa mazoezi ya timu hiyo yanayo endelea kwenye viwanja vya shule ya sekondari Popatlaly mjini hapa,Ofisa Habari wa Coastal Union,Oscar Assenga amesema kikubwa zaidi wanachojivunia ni kuendelea kuimarika kikosi hicho.
Amesema kuwa mipango yake mikubwa ni kuiwezesha timu hiyo kupata matokeo mazuri katika mechi zote zilizosalia ikiwemo kuwataka wachezaji kutimiza wajibu wao wa kuipa ushindi timu hiyo.
Amesema kuwa dhamira yao kubwa ni kupambana kufa na kupona ili kumaliza ligi hiyo wakiwa nafasi tatu za juu kwenye michuano hiyo ambayo msimu huu imeonekana kuwa na upinzani mkubwa.
Hata hivyo amewataka mashabiki pamoja na wapenzi kujitokeza kwa wingi
katika michezo yao iliyosalia ikiwemo ya ugenini na nyumbani ili kuipa
hamasa timu hiyo kufikisha malengo yao

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages