Timu
ya Taifa ya Tanzania ya Wanawake (Twiga Stars) ijumaa ya tarehe 10,
Aprili mwaka huu, itashuka dimbani Uwanja wa Taifa jijini Dar es
salaam kuwakarisbisha timu ya Taifa ya Wanawake ya Zambia (The
She-Polopolo).
Twiga Stars inayonolewa na kocha
mkuu Rogasian Kaijage iliingia kambini mwishoni mwa wiki na kikosi cha
wachezaji 25 katika hostel za TFF zilizopo Karume, kujiandaa na mchezo
huo ambao ni muhimu wa kuwania kufuzu kwa fainali za michezo ya Afrika
mwaka huu.
Katika mchezo wa awali uliofanyika
wiki mbili zilizopita jijini Lusaka Zambia, Twiga Stars iliibuka na
ushindi wa mabao 4-2, mabao yaliyofungwa na Asha Rashid (2), Shelder
Boniface (1) na Sophia Mwasikili (1).
Mshindi wa jumla katika mchezo huo
atafuzu moja kwa moja kwa fainali za Michezo ya Afrika zitakazofanya
nchini Congo – Brazzavile kuanzia Septemba 13 mwaka huu.
VPL KUENDELEA JUMAMOSI
Ligi Kuu ya Vodacom inatarajiwa
kendelea kutimua vumbi mwishoni mwa wiki katika sita nchini, kwa michezo
minne kucheza siku ya jumamosi na michezo mwiwili kuchezwa siku ya
jumapili.
Jumamosi uwanja wa Kambarage mjini
Shinyanga, Kagera Sugar watakuwa wenyeji wa Simba SC kutoka jijini Dar
es salaam, huku jijini Tanga Coastal Union wakiwakaribisha maafande wa
jeshi la Magereza nchini Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Mkwakwani.
Ndanda FC ya Mtwara watakuwa
wenyeji wa wagonga nyundo timu ya Mbeya City katika uwanja wa Nagwanda
Sijaona, wakati maafande wa Jeshi la Kujenga Taifa Ruvu Shooting
wakicheza na ndugu zao JKT Ruvu katika uwanja wa Mabatin uliopo
Mlandizi.
Siku ya jumapili Stand United
watawakaribisha wakata miwa kutoka Morogoro Mtibwa Sugar kwenye uwanja
wa Kambarage, huku Mgambo Shooting wakiwa wenyeji wa timu ya Polisi
Morogoro kwenye uwanja wa Mkwakani jijini Tanga.
KILA LA KHERI YANGA
Rais wa Shirikisho la Mpira wa
Miguu wa nchini TFF, Jamal Malinzi amewatakia kila la kheri wawakilishi
pekee wa Tanzania kwenye kombe la Shirikisho barani Afrika (CC) Young
Africans, katika mchezo wa marudiano dhidi ya FC Platinum ya Zimbabwe
utakochezwa siku ya jumamosi kwenye uwanja Mandava uliopo Gweru
Bulawayo.
Malinzi amesema Young Africans
hawapaswi kubweteka na ushindi walioupata awali wa mabao 5-1, kikubwa
wanapaswa kwenda kupambana kusaka ushindi ugenini ili kuweza kufuzu kwa
hatua inayofuata ya timu 16.
Endapo Young Africans itafanikiwa
kuwatoa FC Platinum itaingia katika hatua ya 16 bora na itakutana na
mshindi kati ya timu za Benifica de Luanda ya Angola au Etoile du Saleh
ya Tunisia.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269