Breaking News

Your Ad Spot

Apr 27, 2015

YANGA KUTWAA UBINGWA LEO MGONGONI MWA POLISI?



 Kikosi cha Yanga
Ligi kuu ya Tanzania Bara itaendelea mwazoni mwa juma hili (Jumatatu) na swali pekee kwa wapenda kabumbu ni kwamba je Yanga, iliyonzishwa mwaka 1935 itatawazwa kuwa mabingwa wapya?. Jibu litakuwa ndio endapo vijana hao wa jangwani watawafunga Polisi Morogoro katika mechi itakayochezwa leo kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Yanga, wawakilishi pekee katika ukanda wa Afrika ya Mashariki katika michuano ya vilabu barani Afrika ambao watacheza na Etoile du Sahel ya Tunisia mjini Tunis katika mechi ya marudiano ya raundi ya 16 ya michuano hiyo wikiendi hii baada ya sare ya 1-1 jijini Dar es Salaam, wana pointi 52, ambazo kimahesabu hazitaweza kufikiwa na timu yoyote wakati ligi hiyo ikielekea ukingoni mwezi ujao.

Baada ya mechi ya leo, Yanga, ikiwa chini ya kocha Mdachi, ambaye hivi karibuni ameiweka timu hiyo katika wimbi kubwa la ushindi, itabakiwa na mechi mbili tu mkononi na haina cha kupoteza hata ikifungwa kwani tayari imemuweka mwali kibindoni

Hata kama mabingwa watetezi, Azam FC, itafanikiwa kumaliza mechi zake zote za ligi, haitaweza, hata kwa miujiza kuifikia Yanga, ambayo haijashinda taji la ligi kuu kwa zaidi ya miaka 2 iliyopita
 Kikosi cha Azam
Azam, waliokuwa wawakilishi wa kombe la washindi barani Afrika (African Champions league) baada ya kutolewa katika michuano hiyo na vigogo wa Sudan, El-Merreikh, wana pointi 45 katika mechi 23 na hata kama itashinda mechi zake tatu zilizobaki, itakuwa imefikisha pointi 54, pointi moja nyuma ya Yanga kama Polisi watafungwa.

Kwa sasa vita ya nafasi ya pili ili kupata tiketi ya michuano ya kombe la Wawakilishi barani Afrika (Confederation Cup) ipo kati ya mabingwa watetezi, Azam na Simba yenye pointi 41 ikiwa na mechi mbili mkononi.

Simba, iliyonzishwa zaidi ya miaka 70 iliyopita, ikiwa chini ya kocha Mserbia, Goran Kopunovic ina Sali na kuomba du azote ili Azam iweze kuteleza katika mechi zake zilizobaki ili irudi katika chati ya michuano ya kimataifa, baada ya kuwa nje mwa miaka kadhaa.

Endapo Yanga watafanikiwa kuchukua ubingwa, wataiwakilisha Tanzania katika michuano ijayo ya kombe la Washindi barani Afrika

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages