Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni na
Mlezi wa Jumuiya ya Tanzania Yuoth Icon (TAYI) Mhe.Eng Hamadi Yussuf
Masauni akikabidhiwa Cheti cha Mchango wake kwa Vijana kuhusiana na
Amani kutoka kwa Mratibu wa UNESCO kwa Vijana Tanzania Ndg Simba Mwinyi
Simba kwa kutambua mchango wake kwa Vijana Zanzibar kudumisha amani,
hafla hiyo mefanyika katika Kituo cha Vijana cha TAYI muembemadema
Zanzibar
Mhe.Eng Hamad Masauni akionesha Cheti baada ya kukabidhiwa wakati wa Kongamano la Vijana wa TAYI baada ya kukabidhiwa,
Naibu Katibu wa Vijana wa Umoja
wa Mataifa Tanzania(YUNA) Bi, Pili Khamis, akikabidhi Cheti
kilichotolewa na YUNA kwa kuthamini Mchango wake kwa Vijana Zanzibar
Mhe.Eng Hamad Yussuf Masauni, makabidhiano hayo yamefanyika katika jengo
la Ofisi za TAYI muembemadema Zanzibar kushoto Mratibu wa YUNA Zanzibar
Ndg Ali Hemed.
Mhe.Eng. Masauni akioneshga Cheti chake baada ya kukabidhia kilichotolewa na YUNA kujali mchango wake kwa Vijana Zanzibar.
Vijana wa Kituo cha TAYI
wakifuatilia hafla hiyo ya makambidhiano ilioendana na Kongamano la
Vijana kuhusiana na Amani Zanzibar wakati wote, Kongamano hilo
limetayarishwa na Unesco kwa kushirikiana na Jumuiya ya TAYI.
Mhe Eng.Hamad Yussuf Masauni,
akizungumza na Vijana wakati wa hafla ya kukabidhiwa Vyeti ilioendana na
Kongamano la Vijana kuhusiana na Amani Zanzibar lililowashirikisha
vijana wa TAYI na wa Vyuo Vikuu Zanzibar lililofanyika katika Kituo cha
TAYI Muembemadema Zanzibar na kudhaminiwa Unesco.
Mratibu wa Unesco Tanzania kwa
Vijana Ndg Simba Mwinyi Simba akizungumza wakati wa Kongamano hilo la
Mafunzo ya kudumisha Amani kwa Vijana Tanzania lililofanyika katika
kituo cha Vijana cha TAYI muembemadema Zanzibar na kushirikisha Vijana
kutoka Vyuo Vikuu Zanzibar na Mabalozi wa Vijana wa Amani.
Mratibu wa YUNA Ndg Ali Hemeid akizungumza na kutowa mafunzo kwa Vijana walioshiriki Kongamano hilo.
Mhe Eng. Hamad Yussuf Masauni,
akiwa katika picha ya pamoja na Vionhozi wa Vijana na Mabalozi wa Amani
wa Vijana Zanzibar baada ya kumalizika kwa Kongamano hilo na kumkabidhi
Chrti Mhe Masauni cha kujali Ushiriki wake kwa Vijana dhidi ya Amani.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269