Nguli wa soka wa timu ya taifa ,Uholanzi na vilabu vya Ajax na
Barcelona,Johan Cruyff (Kulia) akiongozana na mwenyeji wake,Rayco
Garcia mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa
Kilimanjaro(KIA).
(Na mpiga picha wetu)
…………………………………………………………..
Na Mwandishi wetu,Moshi.
MCHEZAJI wa zamani wa timu ya taifa ya Uholanzi na vilabu vya ,Ajax na
Balcelona,gwiji Johan Cruyff amewasili jana majira ya saa 4:45 za
asubuhi katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kwa
ndege ya shirika la ndege la Qatar Airways.
Baada ya kuwasili uwanjani hapo ,Cruyff akiwa ameambatana na familia
yake alipokelewa na Rayco Garcia ,mratibu wa ziara ya wachezaji wa
zamani wa klabu ya Barcelona ya nchini Hispania watakao cheza mechi ya
kirafiki dhidi ya wakongwe wa soka hapa nchini jumamosi ijayo.
Akizungumza na waandishi wa habari uwanjani hapo,Cruyff alisema
anafurahi kufika Tanzania kwa mara ya kwanza na kwamba amefurahia hali
ya hewa ya Joto ukilinganisha na nchi anayotoka ambayo kwa sasa ni
msimu wa baridi.
Alisema ana matarajio makubwa baada ya kukanyaga ardhi ya Tanzania
ikiwemo kuona wanyama wa aina mbalimbali katika hifadhi ya taifa ya
Serengeti pamoja na kutembelea fukwe za bahari katika kisiwa cha
Zanzibar kabla ya mchezo huo wa kirafiki.
“Nasikia furaha kufika Tanzania,na hali ya hewa ni nzuri,hali ya
joto,tunategemea kutembelea maeneo mengi ya vivutio ,tunaenda kutizama
wanyama katika hifadhi ya Serengeti na baadae kutembea fukwe huko
Zanzibar,tunategemea kuona vitu vingi vizuri.”alisema Cruyff.
Kuhusu mchezo wa Jumamoshi ,Cruyff alisema mashabiki wategemeee
burudani toka kwa wakongwe hao wa Barcelona na kwamba mchezo huo
hautakuwa wa ushindani isipokuwa wataonesha burudani ambayo ni
matarajio ya wengi.
“Kitu cha kwanza ni kwamba mashabiki watapata Burudani,hatutacheza ili
kushinda ingawaje tutapenda kushinda ,lakini kikubwa ni kutoa burudani
kwa mashabiki,wafike tu uwanjani kufurahia mchezo”alisema Cruyff.
Cruyff ambaye ni mshindi mara tatu wa tuzo ya Ballon d’O ,1971,1973
na 1974 aliwataka wachezaji wa Tanzania kujituma katika mazoeizi ni
kuzingatia maelekezo ya walimu ili kujenga morali ya timu na wachezaji
kwa ujumla.
“Naweza sema kwa wachezaji pekee ,wanapaswa kufanya mazoezi kwa
bidii,wajaribu kujiweka vizuri kila mara,na kitu kizuri katika michezo
ni umoja wa timu ,mkishinda mnashinda pamoja na mkipoteza mnapoteza
pamoja”alisema Cruyff.
Kuelekea katika Pambano la Jumamosi tayari waratibu wa mashindano hayo
walisema maandalizi yanaendelea vizuri na kwamba baadhi ya wachezaji
wa Barcelona watakao shuka uwanjani siku hiyo ni pamoja na wakongwe
Edaga Davis ,Deco,Patrick Kluivert na Simao Sabrosa.
Historia fupi ya Cruyff.
Mdachi Hendrik Johannes Cruijff alizaliwa Aprily 25 mwaka 1947 katika
jiji la Amsterdam nchini Uholanzi, akajulikana kama Johan Cruyff
ambaye hadi sasa ni meneja wa klabu ya Catalonia ya nchini Hispania.
Cruyff ni miongoni mwa wachezaji maarufu walio anzisha falsafa ya
“Total Football”ambayo ilienea kote duniani hatua iliyopelekea kuwa
mmoja wa wachezaji wenye sifa kubwa katika historia ya soka duniani.
Cruyff alikiongoza kikosi cha timu ya taifa ya Uholanzi katika fainali
za kombe la dunia la Fifa ,mwaka 1974 ambapo alifanikiwa kupata zawadi
ya mpira wa dhahabu baada ya kuibuka mchezaji bora wa mashindano.
Amewahi kuwa kocha wa vilabu vya Ajax na Barcelona kwa nyakati tofauti
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269