Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Takwimu Rwanda Bw.
Yusuf Murangwa akitoa mchango wake kuhusu umuhimu wa ushirikiano wa
matumizi ya Takwimu baina ya nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki leo jijini Dar es salaam.
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Takwimu ya Burundi Bi. Jeanine Niyukuri
akichangia wakati wa mkutano wa Wakurugenzi wa Takwimu wa Nchi
Wanachama wa Jumuiya ya Afriki Mashariki uliofanyika leo jijini Dar es
salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), kutoka Tanzania Dkt. Albina Chuwa akifungua
mkutano wa Wakurugenzi na Watalaam wa Takwimu kutoka nchi Wanachama wa
Jumuiya ya Afrika Mashariki kujadili mausuala mbalimbali ya Takwimu leo
jijini Dar es salaam.
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Takwimu ya Burundi Bi. Jeanine Niyukuri
akichangia wakati wa mkutano wa Wakurugenzi wa Takwimu wa Nchi
Wanachama wa Jumuiya ya Afriki Mashariki uliofanyika leo jijini Dar es
salaam.
Baadhi
yaWashiriki wa Mkutano waWataalam wa Takwimu wanchi Wanachama wa
Jumuiya ya Afrika Mashari ki wakifuatilia mausuala mbalimbali wakati wa
Mkutano huo leo jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisiya Takwimu Kenya Bw.Zachary
Mwangi akizungumza na washiriki wa mkutano wa Wakurugenzi wa Takwimu wa
Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu utayari wa nchi
yake katika matumizi ya Takwimu mbalimbali.
Na Veronica Kazimoto
Dar es Salaam
2/4/2015
Wakurugenzi
Wakuu wa Ofisi za Takwimu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki kutoka Rwanda, Uganda, Kenya, Burundi na Tanzania wamekutana
leo jijini Dar es salaam kujadili
mchango wa matumizi ya Takwimu sahihi katika kuleta maendeleo na kukuza
ushirikiano baina ya Nchi Wanachama wa Jumuiya hiyo.
Akifungua
Mkutano huo Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu kutoka
Tanzania Dkt. Albina Chuwa amesema kuwa mkutano huo pamoja na mambo
mengine unazileta pamoja Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
kujadili na kubadilishana uzoefu kuhusu masuala mbalimbali ya Takwimu na
mchango wake katika kukuza uchumi na kuleta maendeleo ya nchi hizo.
Amesema
kuwa mkutano huo umelenga kuongeza na kuimarisha ushirikiano baina ya
Nchi Wananchama wa Jumuiya hiyo katika matumizi ya Takwimu pamoja na
kupitia mabadiliko ya sheria mbalimbali zinazosimamia masuala ya Takwimu
kwa Nchi Wanachama.
Kwa
upande wao wakurugenzi hao kutoka Rwanda, Uganda, Kenya, na Burundi
wakizungumza kwa nyakati tofauti wamesema kufanyika kwa mkutano huo
nchini Tanzania kunatoa matumaini ya mwendelezo wa ushirikiano katika
matumizi ya takwimu sahihi kutokana na mchango wake katika maendeleo ya
nchi zao na Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa ujumla.
Wamesema
kuwa nchi zao zitaendelea kushirikiana kikamilifu katika kuhakikisha
kuwa kunakuwa na usimamizi mzuri wa takwimu mbalimbali zikiwemo za
kilimo, Viwanda, Biashara, uchumi na takwimu nyingine kwa manufaa ya wananchi wa Jumuiya hiyo.
Kufanyika
kwa mkutano huo nchini Tanzania ambao umehusisha wakurugenzi wakuu,
wakurugenzi na maafisa wandamizi wa takwimu ni mwendelezo wa mikutano
mbalimbali inayofanyika katika Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki kwa ajili ya kujadili mchango wa matumizi ya Takwimu sahihi
katika kuleta maendeleo na kukuza ushirikiano baina ya Nchi Wanachama wa
Jumuiya hiyo.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269