Breaking News

Your Ad Spot

Apr 3, 2015

STAR TIMES KUTOA TUZO YA PIKIPIKI KWA WATEJA WAKE

*Yazindua droo ya Bahati nasibu ya mwezi Aprili

Makamu wa Rais wa kampuni ya StarTimes Tanzania, Bi Zuhura Hanif (kulia) akichomeka ufunguo wa pikipiki wakati wa uzinduzi wa droo ya bahati nasibu ya mwezi wa Aprili ambayo kila wiki pikipiki moja itashindaniwa. Akishuhudia tukio hilo kushoto ni mwandishi wa kituo cha luninga cha Channel Ten, Fred Mwanjala. Kujiunga na bahati nasibu hiyo wateja wa StarTimes wanatakiwa kulipia kifurushi kuanzia shilingi 10,000/- na kuendelea.
Makamu wa Rais wa kampuni ya StarTimes Tanzania, Bi Zuhura Hanif  akiweka pozi mbele ya pikipiki wakati wa uzinduzi wa droo ya bahati nasibu ya mwezi wa Aprili ambayo itahusisha wateja wote wa kampuni hiyo nchini. Kujiunga na bahati nasibu hiyo wateja wa StarTimes wanatakiwa kulipia kifurushi kuanzia shilingi 10,000/- na kuendelea.
Makamu wa Rais wa kampuni ya StarTimes Tanzania, Bi Zuhura Hanif  akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa droo ya bahati nasibu ya mwezi wa Aprili ambayo itahusisha wateja wote wa kampuni hiyo nchini. Kujiunga na bahati nasibu hiyo wateja wa StarTimes wanatakiwa kulipia kifurushi kuanzia shilingi 10,000/- na kuendelea.
Makamu wa Rais wa kampuni ya StarTimes Tanzania, Bi Zuhura Hanif  akifurahia jambo na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa droo ya bahati nasibu ya mwezi wa Aprili ambayo itahusisha wateja wote wa kampuni hiyo nchini. Kujiunga na bahati nasibu hiyo wateja wa StarTimes wanatakiwa kulipia kifurushi kuanzia shilingi 10,000/- na kuendelea.

Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam
·  ILI kujiunga na droo hii ya bahati nasibu wateja wanatakiwa kulipia malipo ya kifurushi kuanzia Sh. 10,000/- tu na kuendelea ambapo kila wiki pikipiki moja itatolewa kama zawadi.
Dar es Salaam, April 2, 2015 … Katika kuwajali na kuwakumbuka wateja wake kampuni ya huduma ya matangazo ya luninga kwa dijitali nchini, StarTimes leo imezindua droo ya bahati nasibu inayokwenda kwa jina la ‘Vuka Boda na StarTimes’ kwa wateja wake ambapo kila wiki itakuwa ikitoa pikipiki moja kama zawadi.

Akitoa ufafanuzi juu ya droo hiyo, Makamu wa Rais wa StarTimes Tanzania, Zuhura Hanif amesema kuwa droo hii ya bahati nasibu itakayochezeshwa ndani ya kipindi chote cha mwezi wa April inahusisha wateja wao wote.

“Tunayo furaha kuwatangazia kuwa StarTimes imewaletea wateja wake droo ya bahati na kujishindia pikipiki. Jumla ya pikipiki zitakazoshindaniwa ni nne na zitakuwa zikitolewa kwa mshindi kila wiki baada ya droo kuchezeshwa. 

Droo hii itahusisha wateja wote wa kampuni popote walipo, iwe ni Dar es Salaam au mikoani, tutahakikisha mshindi anapatiwa pikipiki yake. Ili kushiriki na kuibuka na pikipiki itambidi ajiunge na kifurushi cha malipo ya kuanzia shilingi 10,000/- tu na kuendelea ambapo nambari ya kadi yake ya kisimbuzi ndiyo itakayotumika kushindanishwa.” Alifafanua Bi Hanif
“Dhumuni la droo hii ya mwezi ya bahati ni kurudisha fadhila kidogo kwa wateja wetu ukizingatia tutakuwa na mapumziko mafupi ya sherehe za Pasaka nyumbani na familia zetu. 

Katika mapumziko haya tunataka wateja wote wa StarTimes walipie vifurushi vyao kuburudika huku wakisubiria kushinda zawadi ya pikipiki.” Alisema Bi Hanif na kuongezea, 

“Tunafahamu kuwa pikipiki ni chombo muhimu kwa usafiri na vilevile ni njia mojawapo ya kujiingizia kipato hivyo tunaamini itakuwa ni msaada mkubwa kwa wateja wetu.”

Aliendelea kwa kusema kuwa StarTimes imekuwa ikiwapatia huduma na bidhaa nzuri kwa kipindi kirefu sasa na siku zote inajitahidi kuziboresha kwa kuwasikiliza wateja wanataka nini.
“Katika kuhakikisha tunakidhi haja za wateja wetu, StarTimes inajitahidi kwa kiasi kikubwa kuongeza channeli na vipindi vinavyopendwa na watu wengi. 

Mfano mzuri hivi karibuni tumeongeza chaneli ya michezo ya ‘StarTimes Sports Focus’ katika kisimbuzi chetu. Chaneli hii inahusu michezo, uchambuzi, makala na habari za michezo mbalimbali ikiwemo soka, masumbwi, mieleka na mingineyo. 

Hivyo kwa wale wapenda michezo nawashauri msipitwe na hii chaneli huku nyingine nyingi zikiwa njiani kuunganishwa.” Alielezea
Kwa kuhitimisha Bi Hanif amewataka wateja wote kuchangamkia hii fursa kwa kujiunga na vifurushi kwa shilingi 10,000 na kuendelea ili kuingia katika droo na kushinda kwani bahati inaweza kumuangukia mtu yeyote na kubadili maisha yake kutokana na zawadi hii.


Wateja wanakumbushwa wanaweza kulipia vifurushi kwa njia mbalimbali zikiwemo za vocha zinazouzwa katika ofisi na mawakala wa kampuni zaidi ya 800 katika mikoa 17 tuliyopo ambapo mteja atapiga *150*63# na kufuata maelekezo. 

Kulipia kupitia simu zao za mikononi kama vile Tigo-Pesa, M-Pesa, Airtel Money, Maxcom, Selcom pamoja na huduma za mobile-benki zilizounganishwa na huduma hii.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages