Dennis Ssebo Kutoka kituo cha
redio cha EFM akizungumza na mgeni rasmi Mkuu wa mkoa wa Sar es salaam
Mh. Meck Sadick wakati wa promosheni ya shindano la Shika Ndinga
iliyofanyika kwenye viwanja vya Tanganyika Parkers Kawe jijini Dar es
salaam kulia ni Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Mh. Paul Makonda.
………………………………………………………………….
Hatimaye Washindi washindano la
shika ndinga la 93.7 EFM wapatikana baada ya mchuano mkali uliofanyika
jana tarehe 25 mwezi wanne katika viwanja vya Tanganyika pakers kawe.
Fainali hiyo ilihusisha washiriki kumi kutoka katika wilaya 3za mkoa wa
dar-es-salaam kumi tano kati yao wakiwa wanawake na kumi na tano wakiwa
ni wanaume.
Shindano hilo lilihudhuriwa na
mkuu wa mkoa mheshimiwa Sadiq Mecky Said akiwa kama mgeni rasmi, mkuu wa
wilaya ya kinondoni mheshimiwa Paul Makonda na naibu meya wa wilaya ya
temeke mheshimiwa Jumma mkenga.
Akiongea jana mheshimiwa Sadiq
Said alisema ni ubunifu wa hali ya juu ulioneshwa na kituo cha 93.7 EFM
kwa kuanzisha shindano la aina yake ambalo litaongeza ajira kwa vijana
na kuinua hali zao za uchumi ,pia aliwahasa washindi kutumia ndinga
walizoshinda ili kujiendeleza kiuchumi. Kwa upande wake mheshimiwa Paul
Makonda alisema vijana wajifunze kujitokeza katika mashindano kama haya
maana zaidi ya kuburudisha yanabadilisha maisha yao kwa namna yatofauti.
Washindi waliojishindia ndinga kwa
upande wa wanaume ni Gabriel Robert kutoka wilaya ya temeke mwenye umri
wa miaka 36 na Stella Joseph kutoka wilaya ya ilala mwenye umri wa miak
26 ambao kwa pamoja wamesema shindano halikuwa rahisi na wanafuraha
kubwa ya kujishindia gari hizo ambazo watazitumia katika biashara zao
aidha wameishukuru redio ya 93.7 EFM kwa kuandaa shindano hilo na
kuwashauri wasikilizaji waendelee kusikiliza redio hiyo maana inajali
wasikilizaji wake.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269