Na Victor Melkizedeck Abuso
Marekani
imelaani hatua ya rais wa Burundi Piere Nkurunziza kutangazakuwania
urais kwa muhula wa tatu wakati wa uchaguzi Mkuu mwezi Juni mwaka huu.
Msemaji
wa Mambo ya nje wa Marekani Marie Harf amesema hatua ya chama tawala
CNDD FDD kumwidhinisha rais Nkurunziza ni ishara kuwa Burundi inapoteza
nafasi ya kuimarisha demokrasia yake.
Marekani
imewaomba wananchi wa Burundi kusalia watulivu na kuwataka wanasiasa
kuhakikisha kuwa uchaguzi Mkuu unakuwa huru na haki na kusisitiza kuwa
inafuatilia kwa karibu hali ya kisiasa nchini humo.(P.T)
Siku ya Jumamosi Mwenyekiti wa chama tawala Pascal Nyabenda alisema,
"Tungependa kulitangazia taifa na Jumuiya ya Kimataifa kuwa mwanachama aliyeteuliwa kutuwakilisha katika Uchaguzi Mkuu ni rais Pierre Nkurunziza,".
"Tungependa kulitangazia taifa na Jumuiya ya Kimataifa kuwa mwanachama aliyeteuliwa kutuwakilisha katika Uchaguzi Mkuu ni rais Pierre Nkurunziza,".
Nyabenda aliongeza kuwa," Nkurunziza ana haki ya kuchaguliwa kwa muhula wa tatu,".
Upinzani
na Mashirika ya kiraia yamesema yataanza maandamano leo Jumapili jijini
Bujumbura kulaani hatua ya rais Nkurunziza ambayo wanasema ni kinyume
cha Katiba ya nchi hiyo inayomtaka rais kuwa madarakani kwa mihula miwil
tu kama ilivyokubaliwa katika mkataba wa amani wa Arusha.
Mwanaharakati Pierre Claver Mbonimpa amesema, " Hatua hii haikubaliki, inakeuka katiba ya nchi,".
Umoja wa
Mataifa unasema kuwa zaidi ya watu elfu nane tayari wamekimbilia nchini
Rwanda kwa hofu ya kuzuka kwa machafuko ya kisiasa nchini humo.
Kuna hofu
kuwa, machafuko yaliyoshuhudiwa kati ya mwaka 1993 hadi 2006 yakarejea
tena baada ya rais Nkurunziza kutangaza kuwania urais kwa muhula
mwingine.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269