Breaking News

Your Ad Spot

Apr 26, 2015

WENGI WAJITOKEZA KWENYE USAILI WA SHINDANO LA TMT JIJINI MWANZA


Baadhi ya washiriki kutoka Kanda ya Ziwa wakipewa maelekezo kutoka kwa mfanyakazi wa TMT kwa ajili ya kuanza usaili.

Washiriki wa shindano la TMT 2015 jijini Mwanza wakipewa semina elekezi.

Washiriki wakiwa tayari kuingia chumba cha majaji kwa ajili ya kuanza usaili.(P.T)
Na Andrew Carlos/GPL
WASANII wengi ambao wanaamini wana uwezo mkubwa wa kuigiza, wamejitokeza leo ndani ya Isamilo Lounge kufanyiwa usaili katika lile shindano la kusaka vipaji vya kuigiza lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents (TMT).
Akizungumza na mtandao huu, msemaji mkuu wa shindano hilo, Happiness Ntanga alisema kuwa wanashukuru kwa Kanda ya Ziwa kupokelewa vizuri ambapo wengi wameguswa na shindano hilo.
“Niwaambie tu, usaili huu tutaendelea nao mpaka Jumatano ya Aprili 29 na baada ya hapa tutaelekea Kanda ya Kaskazini yaani Arusha hivyo wote wenye vipaji mjiandae,” alisema Ntanga.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni Mpaka Kieleweke ambapo Mei 6, mwaka huu kutakuwa na uzinduzi wa filamu iliyojumuisha wale wakali walioingia 10 bora msimu wa kwanza.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages