Breaking News

Your Ad Spot

Apr 24, 2015

YANGA YAITANDIKA MKONO RUVU SHOOTING,POINTI TATU BADO KUTANGAZWA UBINGWA RASMI

Dada wa Yanga akiwa na kombe bandia
Yanga imebakiza pointi tatu kutangaza ubingwa rasmi baada ya kuendelea kujiweka kwenye nafasi nzuri kufuatia ushindi mnono walioupata leo kwenye uwanja wa Taifa na kufikisha pointi 52.

Yanga ambao mpaka  sasa wamebakiza mchezo mmoja kuhitimisha ratiba ya ligi kuu Tanzania bara, ikitokea wakapata ushindi watakuwa wamefikisha jumla ya pointi 55 ambazo haziwezi kufikiwa na mabingwa watetezi Azam wala timu nyingine yoyote.
Katika mchezo wa leo katika Uwanja wa Taifa Dar, YANGA imeibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Maafande wa Ruvu Shooting, mchezo huu ulionekana kuchezwa upande mmoja, huku Ruvu Shooting wakionekana kuzidiwa kila idara na kuwapa nafasi washambuliaji wa Yanga wakiongozwa na Msuva kutawala mpira kwa kiasi kikubwa.
Yanga walianza kupachika magoli dakika ya 13 kupitia kwa Simon Msuva ambaye alifunga kwa kichwa akiunganisha krosi safi ya Niyonzima kabla ya Sherman kupachika goli la pili.
Dakika ya 45 kabla ya kwenda mapumziko Msuva tena akawainua mashabiki wa Yangakwa kufunga bao la tatu.
Katika kipindi cha pili Tambwe alianza tena kuwainua mashabiki wa Yanga dakika ya 58 kwa kufunga bao la nne baada ya mabeki wa Ruvu kujichanganya na yeye kumalizia shuti.
Dakika ya 67 Sherman anahitimisha ushindi mnono kwa Yanga kufuatia likiwa ni bao la tano kwa kichwa krosi nzuri ya Abdul Juma.
Yanga SC Vs Ruvu Shooting
Haruna Niyonzima (kushoto), Simon Msuva (kulia) na Kpah Sherman wakishangilia baada ya Simon Msuva kuipatia timu hiyo bao la pili.

Yanga SC Vs Ruvu Shooting
Mshambuliaji wa Yanga, Kpah Sherman, akishangilia bao

Yanga SC Vs Ruvu Shooting

Mshambuliaji wa Yanga, Amis Tambwe akiwatoka wachezaji wa Ruvu Shooting

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages