Kiongozi mkuu wa chama cha Alliance for Change and Transparency ACT Wazalendo Zitto Zuberi Kabwe
UKWASI wa
Kiongozi Mkuu wa Chama Cha Alliance for Change and Transparency(ACT
Wazalendo), Zitto Kabwe umeongezeka kutoka umiliki wa shamba moja na Sh milioni 30 alizokuwa amezihifadhi katika
akaunti
za benki mbili tofauti hapa nchini, na sasa anamiliki mali na fedha
zinazofikia Sh milioni 690, MTANZANIA Jumamosi linaripoti.
Kwa
mujibu wa taarifa hizo mpya alizoziweka hadharani wiki hii katika fomu
maalum ya kuonyesha mali zinazomilikiwa na viongozi wa chama hicho,
Zitto ametanabaisha kuwa kwa sasa anamiliki nyumba mbili.
Nyumba
hizo, moja ina thamani ya Sh milioni 180 na nyingine Sh milioni 43, Pia
anamiliki kitalu cha ekari 12 ambacho kinathamani ya Sh milioni 25,
vyote vikiwa Mwandiga mkoani Kigoma.
Zitto pia ameweka hadharani kumiliki mashamba matatu katika mikoa ya Kigoma, Mtwara na Dar es Salaam.
Katika
ufafanuzi wake kuhusu mashamba hayo, Zitto ameeleza kuwa anamiliki
shamba la ekari sita katika manispaa ya mji wa Mtwara likiwa na thamani
ya Sh milioni 60.
Hali
kadhalika shamba lingine la ekari tatu lenye thamani ya Sh milioni 20
huko Matyazo Kigoma, lingine la ekari 3 lenye thamani ya shilingi
milioni 90 ambalo liko Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Katika
fomu hiyo, Zitto alijaza kuwa anamiliki pia gari moja aina ya Land
Lover, Free Lander ambalo alinunua kwa dola za Kimarekani 40,000 sawa na
Sh. milioni 72.
Kwa
upande wa fedha alizokuwa nazo wakati anajaza fomu hiyo ni Sh. milioni
18, pia alitanabaisha kuwa amehifadhi fedha katika Benki ya CRDB, NMB na
STANBIC zenye jumla ya Sh milioni 9.8.
Zitto pia
aliweka wazi kumilika shirika lisilo la kibiashara la Kigoma
Development Initiatives ambalo linaumiliki wa vitalu vya maili 25 huko
Ilogelo wilaya ya Uvinza.
Pamoja na hilo pia anamiliki Kampuni ya Gombe Advisors ambayo inahisa asilimia 25 katika Kampuni ya Leka Dutigite.
Zaidi ameeleza kuwa ameanza kuchangia mfuko wa Hifadhi za Jamii(NSSF), tangu mwaka 2004.
Mbali na
hilo la ukwasi, Zitto alieleza bayana juu ya madeni aliyoyakopa kwa
nyakati tofauti wakati akiwa mbunge, ambayo yana jumla ya Sh. milioni
174.6.
Kwa
nyakati tofauti, Zitto amekuwa akihusishwa na kuwa na ukwasi wa hali ya
juu yakiwamo magari ya kifahari jambo ambalo amekuwa akilikanusha.
Mwaka
2012 alikaririwa na vyombo vya habari pasipo kutaja thamani, alisema
kuwa anamiliki nyumba yenye vyumba viwili huko Kigoma.
"Sijawahi
kuwa na nyumba wala kiwanja hapa Dar wala Dodoma isipokuwa nyumbani
Kigoma, huko nina nyumba ya vyumba viwili tu ambayo niliijenga wakati wa
uchaguzi baada ya wazee kunishauri kuwa siyo vizuri kuendelea kutumia
nyumba ya baba yangu...Nina akaunti mbili tu moja benki ya NMB na
nyingine benki ya CRDB na zote hazina fedha zaidi ya shs Mil. 15 kila
moja." Alikaririwa wakati huo.
Pia
alitoa utetezi wake wa umiliki wa magari, ambapo alisema kuwa anamiliki
gari aina aina ya Land Lover, Free Lander pamoja na gari dogo aina ya
Toyota Vista.
"Baada ya
kuwa mbunge , nakumbuka April 2007 niliingiza nchini gari aina ya
Hammer na nadhani nilikuwa mtu wa pili kuingiza gari hilo hapa nchini,
Kaka yangu Salum anayefanya biashara ya magari ndiye aliyeniletea na
hili sikuliendesha zaidi ya wiki mbili, likanishinda. Lilikuwa la
kifahari mno, nikamwambia alichukue aliuze na hela yangu anirudishie,"
alikaririwa Zitto. CHANZO: MTANZANIA (Muro)
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269