Mwenyekiti
wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) ambaye pia ni Meya wa
Jiji la Dar es Salaam, Dk. Didas Masaburi (katikati), akizungumza na
waandishi wa habari jijini jana kuhusu Mkutano Mkuu wa 31 wa ALAT
utakaokwenda sambamba na Tuzo za Viongozi wa Serikali za Mitaa ‘Mayors
Award’ na Miaka 30 ya ALAT, utakaofanyika katika hoteli ya Kunduchi
jijijni Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu wa ALAT, Habraham
Shamumoyo na (kulia) ni Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya NMB ambao ndio
wadhamini wakuu wa mkutano huo, Waziri Barnabas.
Afisa
Mkuu wa Fedha wa Benki ya NMB, Waziri Barnabas (kushoto), akikabidhi
mfano wa hundi ya shilingi milioni 200, kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya
Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) ambaye pia ni Meya wa Jiji la Dar es
Salaam, Dk. Didas Masaburi kwa ajili ya kudhamini mkutano huo. Katikati
ni Katibu Mkuu wa ALAT, Habraham Shamumoyo.
Jumuiya
ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) itafanya Mkutano wake Mkuu wa 31
katika hoteli ya Kunduchi jijijni Dar es Salaam. Kauli mbiu ya Mkutano
huo unaodhaminiwa na benki ya NMB ni “Wananchi pigia kura katiba
pendekezwa kuboresha Serikali za Mitaa na maendeleo endelevu baada ya
mwaka 2015”“.
Mkutano
mkuu wa 31 unafanyika pamoja na mambo makubwa mawili yafuatayo; Moja ni
Sherehe za Miaka 30 ya Serikali za Mitaa na ALAT ambayo itakuwa na
kongamano la kutathmini tulikotoka, tulipo na kuangalia nini cha kufanya
huko mbeleni ili kuziwezesha Serikali za Mitaa kutoa huduma kwa ufanisi
zaidi.
Pili,
sherehe za tuzo za viongozi bora wa Serikali za Mitaa (Mayors Award).
Kwa mara ya kwanza ALAT itatoa tuzo kwa viongozi wa Halmashauri ambao
wanafanya vizuri katika kusimamia Halmashauri zao. Katika mchakato wa
kuwapata viongozi bora wananchi wameshirikishwa kwa kutuma ujumbe mfupi
kwa njia ya simu kwenda namba 15440.
Kwa
mwaka wa pili mfululizo, NMB wamekuwa wakidhamini mkutano wa ALAT na
kwa mwaka huu, wametudhamini kwa shilingi milioni 200 ambapo milioni 150
ni kwaajili ya matayarisho ya mkutano na milioni 50 kwaajili ya ununuzi
wa trekta ambalo litakabidhiwa kwa washindi wa tuzo ya uongozi bora wa
Serikali za Mitaa (Mayors Award). Trekta hili tunaimani litasaidia
shughuli mbalimbali za halmashauri iliyoshinda kama shughuli za
ukandarasi ikiwemo utengenezaji wa barabara na urekebishaji wa
miundombinu ndani ya halmashauri.
Mkutano wa mwaka huu una umuhimu wa pekee katika historia ya Serikali za Mitaa na taifa letu kwa jumla.
Mwaka
huu ni mwaka wa 31 tangu kurejesha mfumo wa Serikali za Mitaa hapa
nchini mwaka 1984; pili Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania inaadhimisha
miaka 31 tangu kuanzishwa kwake tarehe 13 Disemba 1984. Tatu mwaka huu
nchi yetu inapitia kwenye mchakato wa Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania itakayotuwekea misingi na kanununi za uendeshaji wa nchi
yetu kwa miaka 50 ijayo ikiwa ni pamoja na kuweka mifumo ya Serikali za
Mitaa itakayo jikita kwenye ugatuaji wa madaraka kupeleka kwa wananchi.
Mkutano
Mkuu wa kawaida wa Jumuiya hufanyika mara moja kila mwaka na wajumbe
wake ni: Wenyeviti na Mameya 168 wa Halmashauri za Majiji, Manispaa,
Miji na Wilaya, Wakurugenzi 168 wa Halmashauri, Wabunge 25 mmoja toka
kila mkoa. Mkutano huu utahudhuriwa pia na Wizara, Idara za Serikali
Kuu, Wakala za Serikali, Taasisi shiriki katika Serikali za Mitaa,
wawakilishi wa Balozi na Wabia katika Maendeleo, Mashirika ya Kimataifa
na Jumuiya za Serikali za Mitaa za Afrika Mashariki na wadau wangine wa
sekta ya Serikali za Mitaa.
Aidha
Mkutano huu utahudhuriwa na Asasi zisizo za Kiserikali, Mashirika na
Makampuni na Wawakilishi wa Sekta Binafsi. Inatarajiwa kwamba Mkutano
huu utahudhuriwa na Washiriki takribani mia tano (550). Mkutano Mkuu wa
ALAT ndiyo chombo cha juu kabisa cha maamuzi cha Jumuiya.
Maandalizi
yote kwa ajili ya Mkutanop yamekamilika kwa asilimia 95 na kwa namna ya
pekee Kabisa tumemwalika Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dokta Jakaya Mrisho Kikwete kuwa Mgeni Rasmi wa mkutano wetu
Mkuu pamoja na kutoa tuzo za kwa Mameya/wnyeviti wa Halmashauri.
Niwashukuru
wadau mbalimbali amabo wamejitokeza katika kufadhili na kusaidia
Mkutano huu. Kwa namna ya pekee kabisa niwashukuru benki ya NMB kwa
kuendelea kuwa mwenza (partner) katika Mkutano huu na tuzo za viongozi
wa serikali za Mitaa.
Niwashukuru pia PSPF, MABIBO BEER & WINE, MSD, NHC, NIDA, GF TRUCKS, PPF,TBA, TAA, LAPF, TSN, UTT.
Jumuiya
ya Tawala za Mitaa Tanzania ni chombo kinachoziunganisha Halmashauri
zote za Wilaya, Miji, Manispaa na Majiji Tanzania Bara. Kwa sasa kuna
Halmashauri 168 zinazounganishwa na chombo hiki.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269