Afisa
Uhamiaji wa mkoa wa Arusha Daniel Nanomba akikanusha vikali taarifa za
aliyekuwa Meneja Mauzo wa kampuni ya Tanzanite One,Jaques Beytel
anayedaiwa kutoroshwa
Jaques Beytel anayedaiwa kutoroshwa
Waandishi wa habari wakiwa kazini
Afisa
Uhamiaji wa mkoa wa Arusha Daniel Nanomba amekanusha vikali taarifa za
aliyekuwa Meneja Mauzo wa kampuni ya Tanzanite One,Jaques Beytel
anayedaiwa kutoroshwa na kueleza kuwa mtu huyo alipatiwa notice ya
kuondoka nchi ambapo Juni 10 mwaka huu aliamriwa kuondoka nchi Juni 13
huku akisindikizwa hadi mpaka wa Namanga na si uwanja wa Kia kama
ilivyoelezwa.
Kwa
mujibu wa Taarifa ya Afisa huyo kwa vyombo vya habari amesema kuwa
Maofisa wa Uhamiaji walimkamata Jaques na kumpatia notice ya kuamriwa
kuondoka nchini na si kutoroshwa na kufafanua kua uamuzi huo ulizingatia
taratibu zote za kisheria.
Nanomba
alisema kuwa Raia huyo ambaye ni mzaliwa wa Afrika kusini na alikua
mfanyakazi wa kampuni ya Tanzanite One ambao tumewaita na kuwaonya.
Afisa
huyo amesema kuwa hawamzuii Mwajiri yeyote anayeajiri mtu kutoka nje ya
nchi na hivyo kuwataka waajiri wahakikishe kuwa watu hao wana kibali
cha kufanya kazi nchi vinginevyo watachuliwa hatua kali na kuongeza kuwa
hadi sasa wamewachukulia hatua waajiri watano.
Kwa
kipindi cha Januari hadi sasa tayari wamefanikiwa kuwakamata wahamiaji
haramu 35 katika mkoa wa Arusha huku nchi ya Kenya ikiwa inaongoza kwa
kuwa na idadi kubwa ya wahamiaji hao nchini.
Kati ya wahamiaji hao 35 wako raia wa kenya 13,Ethiopia wanne,Kongo 4,Ghana 4,dachi 3,Marekani mmoja na kutoka nchi nyingine
Pia
wako Watanzania waliochukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na
kuwaajiri watu kutoka nje wasiokuwa na vibali vya kukaa nchini.
(Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269