Mkuu
wa Kitengo cha Risks na Compliance wa Benki ya Exim, David Lusala
(wapili kushoto) akikabidhi hundi ya shilingi milioni 10 kwa Mweka
Hazina wa Tushikamane Pamoja Foundation (TPF), Ana Rupia (wapili kulia),
ikiwa ni sehemu ya msaada wa benki hiyo kupiga jeki miradi ya TPF ya
kuwasaidia wazee wasiojiweza. Wakishuhudia ni Meneja wa Fedha Mwandamizi
wa Benki ya Exim, Issa Hamisi (katikati) na Meneja Masoko Msaidizi wa
Benki hiyo Anita Goshashy
Mkuu
wa Kitengo cha Risks na Compliance wa Benki ya Exim, David Lusala
(wapili kushoto) akionyesha hundi ya shilingi milioni 10 baada ya
kukabidhi hundi hiyo kwa Mweka Hazina wa Tushikamane Pamoja Foundation
(TPF), Ana Rupia (wapili kulia), ikiwa ni sehemu ya msaada wa benki hiyo
kupiga jeki miradi ya TPF ya kuwasaidia wazee wasiojiweza. Wakishuhudia
ni Meneja wa Fedha Mwandamizi wa Benki ya Exim, Issa Hamisi (kulia) na
Meneja Masoko Msaidizi wa Benki hiyo Anita Goshashy (kushoto).
BENKI
ya Exim Tanzania imekabidhi hundi ya shilingi milioni kumi kwa taasisi
ya Tushikamane Pamoja Foundation (TPF) ikiwa na lengo la kusaidia wazee
wasiojiweza wanaoishi katika kaya zaidi ya 40 jijini Dar es Salaam.
Taasisi
hiyo ambayo kwa sasa inasambaza chakula na vitu binafsi kwa kaya 40
jijini Dar es Salaam kila mwezi pia utekeleza miradi mbali mbali ambayo
ni pamoja na matibabu kwa kundi hilo maalum.
Akizungumza
wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika katika makao makuu ya
benki hiyo jijini Dar es Salaam jana, Mkuu wa Kitengo cha Risks na
Compliance wa Benki ya Exim, David Lusala alisema kuwa benki inajua
umuhimu wa kuchangia sehemu ya pato lake kwa jamii, kwa njia ya miradi
ambayo inabadilisha au kuboresha viwango vya kijamii na kiuchumi kwa
jamii.
"Benki
ya Exim imekuwa makini sana katika kusaidia jamii ianyoizunguka. Kama
sehemu ya shughuli zetu za kijamii, leo tunakabidhi shilingi milioni 10
kwa taasisi ya TPF ili kupiga jeki miradi yao iliyoanzishwa ili kusaidia
wazee wasiojiweza na jamii kwa ujumla.
"Nauasa
uongozi wa TPF kuhakikisha kuwa fedha hizi tulizochangia zinaelekezwa
kwenye matumizi yaliyokusudiwa ili kuwawezesha watu wasiojiweza
kufaidika na shughuli zenu zenye malengo mazuri ya kuboresha maisha
yao," alisema Bw Lusala.
Alibainisha
kuwa benki ya Exim itaendelea kuelekeza fedha zake katika kusaidia
miradi ambayo ni chachu ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini ili
kusaidia kuboresha hali ya maisha ya jamii.
Kwa
upande wake, Mweka Hazina wa Tushikamane Pamoja Foundation, Bi. Ana
Rupia ameipongeza Benki ya Exim kwa msaada wake na kusema kuwa fedha
hizo zilizopokelewa na TPF zitaelekezwa katika miradi ambayo tayari
iliyoundwa kwa lengo la kuwasaidia wazee wasiojiweza.
"Tuna
mpango wa kujenga nyumba kwa ajili ya wazee katika kata ya Kwembe,
Wilayani Kinondoni ambayo itakuwa kama makazi ya wazee wasiojiweza.
Nyumba hiyo itatoa urahisi wa wazee hao kupata huduma za matibabu,
usimamizi wa karibu na huduma nyingine za kiubinadamu kwa walengwa.
"Sasa
tunasubiri kibali cha ujenzi kabla ya kuanza kazi ya ujenzi rasmi.
Tunaishukuru Benki ya Exim kwa msaada wao na nazisihi taasisi nyingine
kuiga mfano huu mzuri wa kuigwa,” Bi Rupia alisema.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269