Breaking News

Your Ad Spot

May 27, 2015

DR. MENGI AZINDUA MPANGO WA AIRTEL FURSA 'TUNAKUWEZESHA' JIJINI DAR

Dar es Salaam Mei, 27 2015
Airtel Tanzania imezindua programu mpya iitwayo Airtel Fursa itakayowawezesha vijana kiuchumi ikiwemo kuwapa mbinu mbalimbali zitakazowasaidia kupata maendeleo zaidi katika shughuli zao.

Akizungumza katika uzinduzi wa programu hiyo, Mgeni wa heshima na  mfanyabiashara mkubwa nchini Dokta Reginald Mengi aliipongeza Airtel kwa kubuni program hiyo itakayosaidia vijana nchini huku akitoa wito kwa vijana wote nchini kuikumbatia fursa hiyo ili kuweza kutimiza malengo yao.

“Hii ni Fursa ambayo vijana wanatakiwa kuikumbatia kwa nguvu zote ili wale wote watakaofaidika waweze kuwashawishi wenzao pia katika miaka ijayo,” alisema”

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania Sunil Colaso alisema vijana watanufaika kwa njia mbalimbali na wataweza kujiendeleza kiuchumi na kupunguza suala la ukosefu wa ajira.

“Airtel FURSA itawawezesha vijana toka sehemu mbalimbali nchini, Fursa zitawafikia vijana wengi wenye kiu na ari ya kufanya ambacho wanakiamini na ambao wako tayari kukabili changamoto mbalimbali ili waweze kufikia malengo yao na kubadilisha hali yao kimaisha,” alisema Colaso.

Alisema program hiyo inawalenga vijana wenye umri kati ya miaka 18-24 ambao watapokea misaada ya vifaa au thamani ili kuweza kutimiza malengo yao.

Mbali na kutoa vifaa hivyo, Bw, Colaso alisema zaidi ya vijana wapatao 1500 watapata mafunzo mbalimbali ya kibiashara kila mwaka kupitia program hiyo.

“Watafundishwa kuhusu usimamizi bora wa fedha, namna ya kupata mikopo, namna ya kufugua akaunti benki na mambo muhimu ya kuzingatia katika uendeshaji wa biashara,” alisema Colaso.

Alisema program hiyo itahusisha vijana kutoka Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, Mbeya na Mtwara.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa Airtel Balozi Juma Mwapachu, aliwataka vijana kutumia program hiyo ya Airtel Fursa kujiendeleza. Huku akiwaomba watanzania kuwapendekeza vijana wote wanaoona wanafaa kufaidika kwa mradi huo kwa manufaa ya jamii zao.

Ili kijana kushiriki au kufaidika na Airtel Fursa atatakiwa kutuma ujumbe mfupi kwenda kwa namba 15626 na kuweka maelezo yafuatayo:- JIna, Umri, aina ya biashara na eneo.

Pia wanaweza kutuma maombi yao kwa kupitia barua pepe airtelfursa@tz.airtel.com.  ambapo watatakiwa kutuma jina kamili, umri, aina ya biashara na sababu ya kuomba msaada kutoka Airtel.

Maelezo kuhusu program ya Airtel FURSA pia yanapatikana kwenye tovuti ya Airtel www.airteltanzania.com.

“Programu hii itanufaisha vijana ambao tayari wana miradi mbalimbali na sio ambao wanataka kuanzisha,” alisema.

 Mwenyekiti Mtendaji wa makampuni ya IPP Ltd, Dk. Reginald Mengi (wa pili kulia), Mwenyekiti wa Bodi ya Airtel Tanzania, Balozi Juma Mwapachu (wa pili kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Sunil Colaso (kulia) na Menejawa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi wakiwa wameshika bango kama ishara ya uzinduzi wa mpango wa Airtel Fursa ‘Tunakuwezesha’, katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.
 << Mwenyekiti Mtendaji wa makampuni ya IPP Ltd, Dk. Reginald Mengi (wa pili kulia), akikabidhi zawadi ya pasi na meza yake kwa muuza mitumba Rashid Seleman (wa pili kushoto), ambaye ni mmoja wa vijana waliowezeshwa na mpango wa Airtel Fursa ‘Tunakuwezesha’ katika hafla ya uzinduzi wa mpango huo, iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji
wa Airtel Sunil Colaso, Mwenyekiti wa Bodi ya Airtel Tanzania, Balozi Juma Mwapachu (wa tatu kushoto) na Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi.


 Mwenyekiti Mtendaji wa makampuni ya IPP Ltd, Dk. Reginald Mengi (wa pili kulia), akikabidhi zawadi ya mashine ya kutengeneza juisi kwa Abdulkarim Ramadhan (wa tatu kushoto), ambaye ni mmoja wa vijana waliowezeshwa na mpango wa Airtel Fursa ‘Tunakuwezesha’ katika hafla ya uzinduzi wa mpango huo, iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kutoka (kushoto) ni Mkurugenzi
Mtendaji wa Airtel Sunil Colaso, Mwenyekiti wa Bodi ya Airtel Tanzania,Balozi Juma Mwapachu na Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi.

 <<Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi akizungumza katika
hafla ya uzinduzi wa mpango wa Airtel Fursa ‘Tunakuwezesha’, iliyofanyika
jijini Dar es Salaam.


 Mwenyekiti wa Bodi ya Airtel Tanzania, Balozi Juma Mwapachu akizungumza
katika hafla ya uzinduzi wa mpango wa Airtel Fursa ‘Tunakuwezesha’,
iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel, Sunil Colaso akizungumza katika hafla ya
uzinduzi wa mpango wa Airtel Fursa ‘Tunakuwezesha’, iliyofanyika jijini Dar
es Salaam.

Mwenyekiti Mtendaji wa makampuni ya IPP Ltd, Dk. Reginald Mengi
akisalimiana na baadhi vijana waliohudhuria katika hafla ya uzinduzi wa
mpango wa Airtel Fursa ‘Tunakuwezesha’, iliyofanyika jijini Dar es Salaam
jana. Anayeshuhudia (mwenye miwani) ni Meneja wa Huduma kwa Jamii wa
Airtel, Hawa Bayumi.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages